Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kupata nafasi ya kuchangia. Napenda kuipongeza hotuba ya Kambi ya Upinzani; mategemeo yangu Serikali itachukua ushauri uliotolewa na kuufanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali hii ya Awamu ya Tano imekuwa ikijigamba ni Serikali ya kutetea wanyonge. Mchango wangu utakua kwa maswali zaidi. Je bajeti hii ni rafiki kwa wanyonge wanaosema wanawatetea? Je itawasaidia kiuchumi? Wanasema uchumi umekua kwa asilimia saba (7%) lakini wananchi huko nje hali ni mbaya sana, uchumi huu umekuwa mwenye makaratasi tu lakini siyo kwa mtu mmoja mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuendelea tunahitaji siasa safi, watu na ardhi. Je siasa za nchi hii ni rafiki kwa maendeleo? Je, sheria zetu ni rafiki kwa maendeleo? Je, bajeti hii imewasaidia sekta binafsi kwa kiasi gani? Je, tozo zilizopungua kwa kiasi gani zinawasaidia wafanyabiashara ambao hawakufunga biashara zao? Je, mfumo wetu wa kodi ni rafiki kwa wafanyabiashara, hawaoni ni wakati muafaka wa kubadili sheria za kodi? Je, mifumo yetu ya benki ni rafiki kwa wafanyabiashara wakati wanakopa sababu riba zipo juu sana 18-22%? Je, mfumo wa masoko kwa wakulima wetu ambao ni zaidi ya 70% ya wananchi ni wakulima Serikali inawasaidiaje kupata masoko? Unakuta mkulima analima mwenyewe, panda, nunua mbegu, mbolea, dawa, anavuna ikifika wakati wa kuyauza mazao yake mfano mahindi inabidi apate kibali kutoka Serikali. Je, Serikali inamwezeshaje mkulima huyu?

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haipo kabisa serious kumsaidia mkulima mfano fedha za maendeleo ambazo zingetumika hata kuzalisha mbegu bora kupata Maafisa Ugani wengi, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji wakulima waachane na biashara ya kutegemea lini wingu linajaa uanze kilimo? Bado bajeti kwa ajili ya maendeleo haitoki ya kutosha, mfano mwaka 2018/2019 ziliidhinishwa bilioni 98 lakini zinatoka bilioni 41 tu. Sasa kichekesho mwaka huu 2019/ 2020 wameidhinisha bilioni 143.5, hivi kama mwaka jana hazijatoka mwaka huu zitapatikana wapi? Naomba Waziri anipe jibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tujuavyo magonjwa yasiyoambukiza yanakuja kwa kasi kubwa lakini tunaweza kuyazuia kwa kufanya mazoezi, lakini barabara zetu siyo rafiki kwa watembea kwa miguu, mitaro ya maji taka ipo wazi ni mategemeo yangu kutengwa bajeti ili mitaro ifunikwe na watu wafanye mazoezi kupitia huko na hii itaipunguzia Serikali kutibu watu kwa magonjwa yenye kuweza kukingika sababu na hili Hospitali yetu ya Kanda ya Kaskazini KCMC wamejitahidi na kuanzisha kitengo cha treatment ya Saratani, tayari wamepata machines za kuchoma mionzi lakini vifaa hivi lazima viwekwe kwenye chumba maalum (Banker). Ni vizuri Serikali ikajenga chumba hicho sababu hii itasaidia sana kuondoa msongamano kwenye hospitali ya Ocean Road.

Mheshimiwa Naibu Spika, utalii ni kati ya sekta zinazochangia katika pato la Taifa zaidi ya 17%, lakini bado Serikali haijawekeza ipasavyo katika sekta hii, mfano, tunazo fukwe nyingi, Dar es Salaam, Bagamoyo, Tanga, Mtwara. Je Serikali ina mpago gani na utalii wa fukwe? Mfano Sadan National Park bado hapajawekezwa vizuri, shirikisheni sekta binafsi wajenge hoteli, kuwe na bank, Curio Shop na kadhalika.