Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, kwanza nachukua fursa hii kukushkuru wewe kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika hotuba hii. Pili nachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake wote kwa kuandaa na kuwakilisha hotuba hii kwa umakini mkubwa sana. Katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, Shirika la Posta (TPC) napenda kuipongeza Serikali yetu kwa kuendeleza juhudi kubwa za kuendeleza na kuiimarisha Shirika hili, shirika hili ni miongoni mwa mashirika makongwe sana katika nchi hii. Shirika hili linajishughulisha na kazi ambazo ni lazima zifuatiliwe ili kufanikisha kazi hizi mfano, kazi ya posta mlangoni hii kazi inahitaji vitendea kazi vya usafiri ili kufika kwenye eneo husika. Ushauri wangu katika jambo hili ni Wizara kuzidisha juhudi ya kuwatafutia usafiri wa uhakika ili kuweza kukabiliana na ushindani mkubwa uliopo nchini.

Mheshimiwa Spika, Shirika la Mawasiliano Tanzania; shirika hili ni miongoni mwa mashirika muhimu sana katika uchumi wa nchi yetu. Nachukua nafasi hii kuipongeza idadi ya wateja (Active customer) wa huduma mbalimbali, hili ni jambo jema kwa sababu wateja ndio watakaowezesha upatikanaji wa faida katika shirika hili.

Mheshimiwa Spika, kazi za mawasiliano kwa sasa zina ushindani mkubwa sana, mashirika mengi ya binafsi yamejitokeza na yanaendelea kujitokeza, hivyo ni vyema shirika likajipanga ili kukabiliana na ushindani huu.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali iliwezeshe shirika hili ili liweze kukabiliana na mashirika binafsi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.