Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itaweka Mdaki katika Bandari ya Dar es Salaam kwa meli za abiria na mizigo za Azam Sea Link ili kuondoa usumbufu na kero kwa abiria?

Supplementary Question 1

MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Waziri, swali la kwanza; kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amesema kwamba uko mdaki mmoja utafungwa katika eneo la Azam Sea Link, tunataka kujua, ni lini mdaki huu utakwenda kufungwa ili kuondoa adha kwa wananchi wanaotumia eneo hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa vilevile Mheshimiwa Waziri amesema kwenye bajeti ya mwaka huu, wametenga fedha kwa ajili ya kununua midaki mingine. Je, ni midaki mingapi itakwenda kunuliwa kwa ajili ya eneo la Azam Sea Link ili kuendelea kuboresha eneo hili? Ahsante.

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza kuhusu lini, ni ndani ya Mwaka huu wa Fedha 2023/2024.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusu ni midaki mingapi itajengwa kwenye eneo hili ni kwamba hakuna mpango wa kuongeza kwenye eneo la Azam Link kwa sababu tayari umeshapatikana mmoja na kama kutakuwa na uhitaji tutakwenda kwenye maeneo mengine yenye uhitaji mkubwa.