Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kilumbe Shabani Ng'enda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:- Je, hatua zipi zimechukuliwa kuhusu Itifaki ya Forodha kati ya Tanzania na DRC kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki?

Supplementary Question 1

MHE. KILUMBE S. NG’ENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri napenda kupata commitment ya Serikali kwamba wakati tukisuburi kukamilika kwa mchakato wa Itifaki ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kati ya nchi yetu na nchi ya DRC ambayo ni mdau mkubwa wa kibiashara wa nchi yetu; je, Wizara yako ipo tayari kukaa na wafanyabiashara wa Kigoma ili kuwapa elimu ya Itifaki hiyo kurahisisha shughuli za kibiashara baina yetu na DRC?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kilumbe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo tayari kutoa mafunzo na kwa ujumla tayari Serikali imeandaa programu maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo ya wafanyabiashara hao, lakini siyo tu waliopo Kigoma bali nchi nzima.