Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jesca David Kishoa

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itapeleka umeme wa REA kwenye Vijiji 23 Wilayani Mkalama?

Supplementary Question 1

MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Moja ya changamoto kubwa inayopelekea miradi hii ya REA kutotekelezwa kwa wakati ni pamoja na ukosefu wa nguzo. Nataka kusikia kauli ya Serikali imejipangaje kwa ajili ya kutatua changamoto hii?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa kuna makampuni yasiyo na uaminifu katika kutekeleza miradi hii ya REA jambo ambalo linasababisha kuendelea kuchelewesha utekelezaji wa miradi hii, mfano kampuni ya TONTAN ambayo imetumia zaidi ya bilioni 3.8 kinyume na utaratibu. Nataka kujua kauli ya Serikali imekwishachukua hatua gani mpaka sasa dhidi ya kampuni hii?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwenye eneo la nguzo kwa ajili ya usambazaji wa umeme tunaendelea kuvihamasisha na kuviwezesha viwanda vyetu vya ndani kuhakikisha kwamba vinatosheleza soko. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi zimekuwa nyingi na miradi imekuwa mingi na hivyo viwanda vinaonekana kuzidiwa na kazi ambazo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amewezesha zifanyike katika nchi yetu. Hata hivyo, tunajitahidi na viwanda vimekuwa vikizalisha nguzo na kwa sehemu kubwa tatizo huilo limepungua na endapo litakuwa kubwa sana tutahakikisha tunazipata kokote zinakowezekana kupatikana ili hilo tatizo liishe.

Mheshimiwa Spika, kwenye swali la pili, kuhusiana na wakandarasi ambao wanalegalega katika katika utekelezaji wa kazi zao. Kama ambavyo tumekuwa tukisema tunao wakandarasi wa lot kama saba ambao tumekuwa tukikamatana nao kwa nguvu zaidi kuhakikisha kwamba wanakamilisha kazi zao. Vile vile, tumewekeana malengo na mikakati na muda utakapofika endapo watashindwa kukamilisha, basi tutavunja mikataba hiyo ili tuweze kupata watu wengine wa kukamilisha kazi kwa wakati. Hata hivyo, kwa sasa tunaendelea vema katika ambayo tumeweka utaratibu wa kufuatilia siku kwa siku kwa kuajiri wale vijana wetu ambao tumewapeleka katika maeneo yetu ya majimbo na hivyo tunapata taarifa za mara kwa mara na usimamizi unakuwa wa karibu. Tunaamini kazi zitakamilika kwa wakati.

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itapeleka umeme wa REA kwenye Vijiji 23 Wilayani Mkalama?

Supplementary Question 2

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Katika Wilaya ya Namtumbo tuna Vijiji viwili cha Ligunga na cha Msisima chenye Shule ya Sekondari ya Kata ya Msisisima iliyojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 600, kilirukwa katika awamu hii na awamu ya tatu mzunguko wa pili. Vile vile, tuliomba viingizwe na vikapata proof na mkandarasi amefanya survey ameleta…

SPIKA: Mheshimiwa swali lako.

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, je, Serikali lini itampa kibali aendelee kufanya kazi hiyo ya kuweka umeme katika Kijiji cha Msisima na Ligunga?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, vijiji vyote ambavyo havikuwa na umeme vitawekewa umeme na mikataba tuliyokuwa nayo inaisha Desemba, 2023, vile vilivyokuwa kwenye miradi ya awali na vile ambavyo vilikuja kuongezwa vyote vitafanyiwa kazi kwenye scope hii ambayo tunakwenda nayo na vitakamilika katika awamu hii.

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itapeleka umeme wa REA kwenye Vijiji 23 Wilayani Mkalama?

Supplementary Question 3

MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Jimbo la Newala Vijijini lina vijiji zaidi ya 60 ambavyo havijapatiwa umeme. Je, ni lini Mradi wa REA, mzunguko wa pili, utaenda kumaliza tatizo hili? Ahsante.

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, Mradi wa REA, awamu ya tatu, mzunguko wa pili, unaendelea na tunatarajia utakamilika ifikapo Desemba, 2023. Katika Jimbo la Newala Vijijini napo mradi huu utatakiwa ukamilike na vijiji vyote vilivyopo vitapata umeme.

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itapeleka umeme wa REA kwenye Vijiji 23 Wilayani Mkalama?

Supplementary Question 4

MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Spika, nakushuru. Kutokana na mpango wa umeme vitongojini kwa Wilaya ya Tunduru bado haujaanza na kuna taasisi mbili za kidini ambazo hazina umeme na ziko vitongojini. Je, ni lini Serikali itapeleka huduma ya umeme kwenye taasisi hizo?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, tayari Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa fedha za nyongeza za kupeleka umeme katika kilometa mbili za ziada ukiachana na ile moja ambayo tulikuwa nayo katika Mradi wa REA III Round II. Kwa hiyo, naamini katika nyongeza hiyo ya kilomita mbili itazidi kuingia kwenye maeneo ya vitongoji na taasisi hizo zikiwekwa ni za kipaumbele, basi Mkandarasi atafikisha umeme kwenye maeneo hayo kwa kipindi hiki ambacho tumepata nyongeza ya pesa ya kupeleka umeme katika kilomita mbili za ziada ukijumlisha na ile moja ambayo itagusa vitongoji vingi zaidi.

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itapeleka umeme wa REA kwenye Vijiji 23 Wilayani Mkalama?

Supplementary Question 5

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itapeleka umeme katika shule zote za msingi, sekondari na taasisi za dini katika wilaya zote Mkoa wa Kigoma?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, katika mpango wa REA III, Round II, tuliokuwa nao sasa tunafikisha umeme katika vijiji vyote na katika maeneo ya vitongoji baadhi kwa kilomita moja ukiongeza na zile kilomita mbili. Hata hivyo, tayari Serikali inatafuta fedha ya kuhakikisha inapeleka umeme katika vitongoji vyote Tanzania takribani 36,000 ambavyo havina Umeme kwa gharama ya shilingi 6,500,000,000,000. Pesa hiyo itakapokuwa imepatikana taasisi na maeneo mengine yote yanayohitaji umeme yatafikishiwa umeme kulingana na upatikanaji wa fedha ambao tunaamini zitapatikana katika muda mfupi ujao.