Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Capt. (Mst). George Huruma Mkuchika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Newala Mjini

Primary Question

MHE. CAPT. MST. GEORGE H. MKUCHIKA aliuliza:- Mradi wa Maji wa Makonde ulijengwa mapema miaka ya 1950 kwa lengo la kuondoa kero ya maji katika uwanda wa Makonde wenye Wilaya za Newala, Tandahimba na sasa Mtwara Vijijini; lakini mradi huu mitambo yake imechakaa na watumiaji wameongezeka ambapo upatikanaji wa maji kwa Wilaya ya Newala ni 31% tu. Je, Serikali inalifahamu tatizo hilo na inachukua hatua gani kutatua tatizo hili?

Supplementary Question 1

MHE. CAPT. MST. GEORGE H. MKUCHIKA: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali kwa kutambua tatizo la maji Mradi wa Maji wa Makonde na kutenga fedha za kutosha kutokana na mkopo uliopatikana kutoka Serikali ya India. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, la kwanza; kitakachoondoa tatizo la maji Mradi wa Maji Makonde ni utekelezaji wa huu mradi mkubwa wa fedha ambazo tumepata mkopo kutoka India. Ningependa kumuuliza Mheshimiwa Waziri, ni lini utekelezaji utaanza wa huo mradi mkubwa?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, jirani na chanzo cha maji Mitema kama alivyosema Mheshimiwa Waziri ambako kuna maji ya kutosha, kuna mji mdogo wa Kitangari na watu wengi, pana Kituo cha Afya, Chuo cha Ualimu, sekondari mbili, watu wengi sana pale, soko kubwa lakini Mji ule ambao uko kama kilometa tatu tu kutoka chanzo cha maji hawapati maji. Maji yanafika Tandahimba, yanafika Mtwara Vijijini, pale kwenye chanzo cha maji hawapati maji. Je, Serikali inajua tatizo hili na kama inajua tatizo hili inawaahidi nini wananchi wa Mji Mdogo wa Kitangari?

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza ni lini utekelezaji wa huu Mradi wa Makonde kupitia mkopo wa masharti nafuu wa Serikali ya India utaanza.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusaini makubalianoya nchi mbili sasa hivi Serikali mbili zinaendelea na taratibu ili kuweza kufikia kusaini financial agreement, baada ya kusaini financial agreement kwa sababu tayari usanifu upo tutakuwa na muda mfupi sana ku review nyaraka za mradi wa Makonde na kutangaza tender na baadae utekeleji uweze kuanza. Kwa hiyo nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba haitachukua muda mrefu maana yake tatizo lilikuwa ni fedha na fedha zimepatikana kwa hiyo kilichobaki ni taratibu zingine ndogo ndogo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mji wa Kitangari ni kweli. Mji huu uko kilometa tatu na Mheshimiwa Mbunge wewe ni shahidi kwamba nilikuja pale na mpaka nikaja Mji wa Kitangari nikaongea na wananchi. Ni kweli kabisa kwamba maji yanatoka chanzo cha Mitema, bomba linapita Kitangari kwenda Tandahimba. Katika huu mradi mkubwa kwa sababu fedha ni nyingi Tutahakikisha kwamba bomba linatoka chanzo cha Mitema pale linakwenda moja kwa moja eneo la Kitangari.
Kwa hiyo, niwahakikishie wananchi wa Kitangari kwamba tatizo la maji walilokuwa nalo muda mrefu sasa kupitia mkopo huu tunalimaliza. (Makofi)