Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza: - Je, ni lini Serikali itakomesha shughuli za ukataji miti, kilimo na ujenzi karribu na vyanzo vya maji ili kulinda vyanzo vya maji?

Supplementary Question 1

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na sheria zote zilizonukuliwa katika Ofisi ya Waziri. Je, Ofisi hiyo inashirikiana vipi na Ofisi ya TAMISEMI, Ardhi, Kilimo na Mifugo katika kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji vinahifadhiwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa nini Serikali isianzishe tuzo maalum kwa ajili ya vijiji na Kamati za Maji zinazohifadhi vyanzo hivyo kikamilifu? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maryam, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tayari Wizara tunashirikiana na hizi wizara ambazo tunaingiliana kimajukumu na hili tumeendelea kulifanya hasa katika ziara ya Wizara za Kisekta tumekuwa tukiendelea kutoa elimu ya pamoja.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusiana na tuzo maalum kama nimemsikia vizuri. Tuzo maalum ni moja ya vitu ambavyo tunavitoa kwenye Jumuiya za Watumia Maji. Tunatoa tuzo kwa maana ya kuwapa motisha ili kuona kwamba wananchi wanashiriki moja kwa moja kwenye utunzaji wa vyanzo vya maji. Vilevile kama ushauri wa Mheshimiwa Mbunge, kwa niaba ya Waziri, naomba niseme nimepokea, tutaendelea kuongeza nguvu. (Makofi)