Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bahati Khamis Kombo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. BAHATI KHAMIS KOMBO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani na eneo lililoachwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Shehia ya Kengeje – Pemba?

Supplementary Question 1

MHE. BAHATI KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naomba kuuliza swali moja la nyongeza. Mheshimiwa Waziri kwa nini sasa hatuoni umuhimu wa kuweka kambi ya kudumu katika eneo hili hasa tukizingatia miundombinu iliyopo ni rafiki? Ahsante.

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyokwishajibu katika jibu la msingi, eneo hilo ni mahsusi kwa ajili zaidi ya mafunzo ya medani na kwamba kikosi nilichokitaja cha 14KJ, hakiko mbali sana kutoka kwenye eneo hili.

Kwa hiyo haja ya kuanzisha kikosi mahsusi kwenye eneo hilo bado labda pale ambapo itabainika kufanyika hivyo katika siku za mbeleni. Ahsante.