Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ramadhan Suleiman Ramadhan

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN K.n.y. MHE. ALI HASSAN OMAR KING aliuliza: - Je, TRA itasitisha lini kukusanya na kuzirudisha fedha za VAT ilizokusanya kutoka kwenye miamala ya mtandaoni iliyofanywa Zanzibar?

Supplementary Question 1

MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Baada ya majibu mazuri ya Wizara kuhusiana na swali nililouliza, nina swali moja la nyongeza. Ni kwamba kumekuwa na uvumi wa muda mrefu kwamba VAT inayotoka kwenye miamala ya mtandao ya simu inakusanywa na mamlaka moja tu ambayo ni ya TRA. Halafu TRA ndio wanakisia kiwango ambacho wanawapa Zanzibar. Wizara wanasemaje kwenye uvumi huo?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ramadhan Suleiman, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni suala la taaluma tu katika nchi yetu kwa jamii yetu kwamba TRA ndio wanakusanya mapato ya pande zote mbili katika suala la miamala. ZRB wanakusanya kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara ni TRA. Kwa hiyo nichukue fursa hii kuwaagiza TRA na ZRB kuendelea kutoa taaluma kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili wajue makato haya yanakatwa vipi kwa mujibu wa sheria. Ahsante.