Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omar Ali Omar

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Wete

Primary Question

MHE.OMAR ALI OMAR K.n.y. MHE. MOHAMMED SAID ISSA aliuliza: - Je, ni vigezo gani Serikali inavitumia kusamehe kodi ya VAT kwa viwanda mbalimbali nchini ili kuleta usawa kwa wote?

Supplementary Question 1

MHE. OMAR ALI OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; je, ni viwanda vingapi vya wazawa ambavyo vimepata msamaha huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, vimewasaidiaje viwanda hivyo? ahsante sana.

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Omar Ali Omar, Mbunge wa Wete kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli swali la kwanza ni suala la takwimu naomba hili tulichukue tutampelekea kwa maandishi. Swali la pili, ni hakika kabisa viwanda vyote vya wazawa nchini vinapata misamaha kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali.