Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Martin Alexander Mtonda Msuha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. MARTIN M. MSUHA aliuliza:- Wananchi wa Tarafa za Hagati, Mbuji na Mkumbi hawapati matangazo ya Redio ya TBC kutokana na Kituo cha TBC- Songea kutokuwa na uwezo wa kurusha matangazo na badala yake wanapata matangazo ya redio toka nchi jirani ya Malawi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza uwezo wa kurusha matangazo ya kituo cha TBC- Songea ili wananchi wa Tarafa hizo wapate habari kupitia TBC?

Supplementary Question 1

MHE. MARTIN M. MSUHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante! Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa umbali wa kutoka Songea na Mamba Bay - Nyasa bado ni mrefu, Serikali haioni haja ya kufunga mitambo angalau kwenye milima ya Mbuji ili kuongeza usikivu katika tarafa hizo zilizotajwa?

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Answer

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upembuzi uliyofanyika, huu mtambo utakaofungwa Mbamba Bay utakuja kukutana na mtambo uliofungwa hapa Matogolo na kwa pamoja usikivu utaongezeka badala ya kufunga kwenye Kata ya Mbuji kama anavyosema. Ni upembuzi wa Kitaalam umefanyika na hili likifanyika tutaongeza usikivu katika eneo lake na kwa sababu ni matokeo ya utafiti tunaamini hili likifanyika basi hayo ambayo Mheshimiwa Mbunge anayaombea hapa yatakuwa yamefanyika na usikivu utaongezeka.

Name

Richard Mganga Ndassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sumve

Primary Question

MHE. MARTIN M. MSUHA aliuliza:- Wananchi wa Tarafa za Hagati, Mbuji na Mkumbi hawapati matangazo ya Redio ya TBC kutokana na Kituo cha TBC- Songea kutokuwa na uwezo wa kurusha matangazo na badala yake wanapata matangazo ya redio toka nchi jirani ya Malawi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza uwezo wa kurusha matangazo ya kituo cha TBC- Songea ili wananchi wa Tarafa hizo wapate habari kupitia TBC?

Supplementary Question 2

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. TBC na Radio ya Taifa ndiyo visemeo vya Serikali. Je, wakati mnaboresha mitambo, Serikali ina utaratibu gani wa kuwapeleka wafanyakazi wa TBC na Radio ya Taifa kwenda nje kujifunza ili kusudi waendane na teknolojia ya sasa, kuwapeleka nje kwenda kusoma?

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Answer

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Ndassa kwa kazi nzuri anayofanya ya kutetea tasnia ya habari kwa sababu na yeye mwenyewe ana background ya habari. Pili TBC imekuwa na mipango mizuri ya kuwapeleka wafanyakazi wake kwenda kuongeza ujuzi wao nje ya nchi, lakini pia na kuwaalika Wataalam mbalimbali kuja hapa kwa ajili ya kuongeza ujuzi wao. Mfano mzuri, wenzetu wa China wamekuwa wakitusaidia sana, wafanyakazi wengi wanakwenda kujifunza. Hata hivi tunapoongea wako wafanyakazi ambao wanaongeza ujuzi wao China, lakini tunao Wachina ambao wako hapa kupitia ushirikiano wa TBC na Star Times, nao wanaongeza ujuzi wa watu wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaamini program hizi zitaendelea na tutaendelea kuziboresha mara kwa mara ili wafanyakazi wetu waendane na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani.