Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amour Khamis Mbarouk

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbe

Primary Question

MHE. AMOUR KHAMIS MBAROUK aliuliza: - Je, ni kwa nini mizigo ya wasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kwa kutumia meli kubwa inapekuliwa na mbwa badala ya scanner?

Supplementary Question 1

MHE. AMOUR KHAMIS MBAROUK: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nilikuwa naulizia iwapo Serikali inaweza kuthibitisha au inaweza kutuhakikishia kwamba huyu mbwa kwa namna walivyom-train hataweza kupata hicho kichaa cha mbwa, ahsante. (Kicheko)

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali moja la Mheshimiwa Amour Khamis Mbarouk, la nyongeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli eneo hili ambapo kuna meli kubwa za mzigo zinazotoka huku Bara kwenda Zanzibar na kwenda Comoro hususan eneo la Azam Sealink na Lighter Key linahitaji kufungwa mzani mkubwa kwa ajili ya ukaguzi wa mizigo inayokwenda na inayoingia pia Dar es Salaam. Serikali ilikwisha tangaza tenda tangu mwaka jana mwezi wa kumi na bahati mbaya hakuna aliyeweza kukidhi vigezo vya tenda hiyo kwa maana ya scanner ama mdaki ambao tunahitaji kama Serikali. Maana tunahitaji scanner iwe kubwa na kwa maana hiyo sasa, tutatangaza tenda upya tarehe 3 ya mwezi wa pili tuweze kufunga midaki miwili katika eneo hili la Azam Sealink na Lighter Key kwa ajili ya meli kubwa za mizigo zinazokwenda Zanzibar pamoja na Visiwa vya Comoro, ahsante.. (Makofi)