Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, Serikali inachukua hatua gani kudhibiti kuongezeka kwa bei ya mbolea nchini hasa Mkoani Ruvuma?

Supplementary Question 1

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa nina maswali mawili ya nyongeza.

Kutokana na ongezeko kubwa la mbolea katika msimu huo uliopita, Je, sasa hivi Serikali sikivu ya CCM inaweza sasa kwa msimu unaokuja kuweka mpango wa kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima wa mazao ya chakula mahindi na mpunga kwa utaratibu mtakaoona unafaa. (Makofi)

Swali la pili, kwa kuwa wakulima wa mahindi msimu huu wamelima kwa gharama kubwa kutokana na bei ya juu ya mbolea. Je, Serikali inaweza kwa msimu huu wa mavuno ikatangaza bei yake mapema NFRA ili wakulima waweze kupata unafuu au bei dira katika soko la mazao ya mahidi. (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Vita Kawawa ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu bei elekezi ya NFRA immediately baada ya Bunge lako Tukufu kupitisha bajeti na tutakapo table bajeti ya Wizara ya Kilimo na bajeti hiyo kupitishwa na Bunge lako Tukufu NFRA itatoa bei ambayo tutanunulia mazao ya nafaka kutoka kwa wananchi. Kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge wasubiri hiyo itafanywa baada ya Bunge la Bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hoja ya ruzuku ninataka nitumie nafasi hii kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge, maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Samia Suluhu Hassan ni kwamba mwaka ujao wa fedha baada ya Julai Mosi, tumepewa jukumu Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha kukaa chini pamoja kutengeneza muundo wa namna ambavyo tutatoa ruzuku kwenye mbolea na siyo tu kwenye mazao maalum tutatoa ruzuku ya mbolea kwa mazao yote ya kilimo ili kutokurudia makosa yaliyokuwepo huko awali. (Makofi)

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, Serikali inachukua hatua gani kudhibiti kuongezeka kwa bei ya mbolea nchini hasa Mkoani Ruvuma?

Supplementary Question 2

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi.

Kwa kuwa Wizara ya Kilimo iliongezea fungu Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo wadogo, inaonaje kama itatenga percent ya fedha hizo kwa ajili ya kutumia ruzuku ili bei ya mbolea kwenye msimu unaokuja iwe sawa na vile wananchi wamezoea ili kuwaondoa kwenye changamoto na majonzi ambayo wameyapitia katika msimu uliopita kwa mfumko mkubwa wa mbolea ambao wameupata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Condester kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutatumia instrument gani kwa ajili ya kutoa ruzuku. Niwaomba Waheshimiwa Wabunge wasubiri kwamba tumalizane kazi tunayoifanya kati ya Wizara ya Fedha na Wizara ya Kilimo kama tutatuma through TADB, tutatumia mfumo mwingine wowote ule tutalitaarifu Bunge lako Tukufu, uhakika tu ni kwamba kuanzia Julai tutatoa ruzuku kwa ajili ya kushusha bei ya mbolea. (Makofi)

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, Serikali inachukua hatua gani kudhibiti kuongezeka kwa bei ya mbolea nchini hasa Mkoani Ruvuma?

Supplementary Question 3

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi na mimi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Waziri pamoja na bei elekezi ambazo zimekuwa zinatangazwa kila wakati, lakini bado imekuwa haitekelezeki kutoka kwenye Mkoa mmoja kwenda Mkoa mwingine hasa Mikoa ile ambayo ni big five kwa uzalishaji wa chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa changamoto hiyo ya uzalishaji ambayo ilikumba na nchi nyingine zote lakini kuna nchi ambazo bado zilifanya vizuri. Je, upo tayari kwenda kujifunza kwenye nchi ambazo nazo zilipata hiyo changamoto ya COVID lakini bado bei ya mbolea iliendelea kuwa nzuri au yenye unafuu wa kwa wakulima ikiwemo Ethiopia, Zambia, Uganda na maeneo mengine. Mpo tayari kwenda kujifunza kwa kuwa ni jambo jema. (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba wataalam wa Wizara ya Kilimo wamekwenda Rwanda kwenda kuangalia subsidy scheme ya Rwanda inafanya kazi namna gani, wengine wamekwenda Zambia kwenda kuangalia subsidy scheme ya Zambia inafanya namna gani, wengine wamekwenda Malawi wameenda kuangalia subsidy scheme ya nchi hizo inafanya namna gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu niwaambie Waheshimiwa Wabunge ni kwamba jambo la subsidy kwenye nchi linahitaji mambo mawili, moja political will na ninamshukuru Mheshimiwa Rais ameonesha utashi wa kisiasa kuwepo kwa subsidy lakini la pili ni management ya mfumo wa subsidy. Nchi yetu ilikuwa na mfumo wa subsidy ambayo ulikuwa abused lakini ukiutazama mfumo ule ya subsidy uliokuwepo ambao ulikuwa abused it was ni mfumo ambao abuse ilitokana na systematic system ambayo ilitengenezwa na kuanzia na aliyekuwa anausimamia mpaka aliyekwenda kuutekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nataka niwahakikishie tu kwamba Waheshimiwa Wabunge ni kwamba tutafanya mfumo wa utoaji wa ruzuku ambao hautoweza kuturudisha kule ambako tumetokea na utashi wa kisiasa wa Mheshimiwa Rais umeonekana hadharani na tarehe Nne mbele ya Watanzania aliahidi na alitoa agizo. Kwa hiyo, mtuachia tulifanyie kazi tuta- communicate na watanzania na kuwaambia namna gani tunalifanyia kazi hili jambo. (Makofi)

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, Serikali inachukua hatua gani kudhibiti kuongezeka kwa bei ya mbolea nchini hasa Mkoani Ruvuma?

Supplementary Question 4

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kuondoka kwa kampuni ya TLTC hapa nchini kumechangia kudorora kwa soko la Tumbaku.

Je, ni lini Serikali itakamilisha mazungumzo na kampuni hii ili iweze kurudi Tanzania kununua Tumbaku za wakulima na kuongeza tija na ushindani? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu niwaambie wakulima wa Tumbaku na niwaambie Watanzania, kiwanda kilichokuwa cha TLTC na kampuni ya TLTC imenunuliwa na sasa hivi amepatikana mwekezaji mwingine na mwekezaji huyu yupo kwenye hatua za mwisho na mwaka huu kiwanda kile kitafunguliwa. Serikali tunawasaidia wawekezaji wapya kuweza kupata minimum quantity ya tumbaku ili kiwanda kile kifunguliwe, kwa hiyo nataka niwaambie tu wakulima wa tumbaku kilichokuwa kiwanda cha TLTC amerudi sokoni kupitia kampuni nyingine ambayo imeweza kununua kiwanda kile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niwahakikishie tu kwamba kiwanda kile kinafunguliwa na ninaamini msimu ujao wa 2022/2023 uzalishaji na makisio yataongezeka tofauti na tulivyokuwa sasa hivi. (Makofi)

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, Serikali inachukua hatua gani kudhibiti kuongezeka kwa bei ya mbolea nchini hasa Mkoani Ruvuma?

Supplementary Question 5

MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwakuwa Benki hii ya Kilimo imeanzishwa kwa namna ya kuwasaidia wakulima wa Tanzania na hii benki inapatikana katika center ya Makao Makuu.

Je, Wizara ina mkakati gani wa hii benki hata kama itashindikana kwa kila Mkoa angalau iende kwenye kila ukanda wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme jambo moja kwanza ieleweke Tanzania Agricultural Development Bank, siyo Commercial Bank is a Development Bank. Kisera tusitajarajie nami nataka niwe mkweli mbele ya Bunge lako Tukufu. Tusitarajie TADB kuwa na matawi kama alivyo CRDB na NMB, huo ndiyo ukweli. Jukumu la kisera la TADB ni Benki ya Maendeleo ambayo moja ya function yake ni ku- de risk sekta ya kilimo kwa kutoa dhamana kwenye commercial banks, ili commercial banks ziweze kuwakopesha wananchi, hili ni jambo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili tumeitaka TADB iwe na ofisi katika Mikoa na Kanda, sasa hivi Kanda ya Kati wapo, Kanda ya Magharibi wapo, Kanda ya Ziwa wapo, Kanda ya Kaskazini wameshafungua ofisi. Kwa hiyo, wana ofisi zao. Wanachokifanya sasa hivi TADB ni kuwa na makubaliano na commercial banks ambazo zitafanya kazi na wao na wao wanatoa dhamana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie Bunge lako kuwaambia sekta ya kilimo sasa hivi imekuwa ikipata mikopo mingi sana kutokana na guarantee zinazotolewa na Tanzania Agricultural Development Bank. Tunaendelea majadiliano na TADB kuboresha na kufanya awareness kwamba namna gani huduma zao zinaweza kuwepo katika taasisi za benki, katika Mikoa na Wilaya ili angalau wawe na madawati waweze kufanya kazi vizuri na Commercial Banks.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tusidhani kwamba TADB ni kama ilivyo CRDB, NMB ama ilivyo Akiba Commercial Bank hii ni Development Bank ina majukumu yake ambayo yamewekwa wazi. Nasi tunawaomba Waheshimiwa Wabunge tuache kuitaka TADB kwenda Wilaya, bali tui- demand TADB itoe dhamana kwenye Commercial Banks ili wakulima wadogo wadogo wasiokuwa na dhamana waweze kukopesheka kirahisi na Commercial Banks. (Makofi)

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, Serikali inachukua hatua gani kudhibiti kuongezeka kwa bei ya mbolea nchini hasa Mkoani Ruvuma?

Supplementary Question 6

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kumuuliza Waziri swali la nyongeza kwamba kumekuwepo na malalamiko kwa wananchi kuhusu ubora wa mbolea zinazoingizwa nchini na makampuni mbalimbali hasa mahindi na mazao ya kunde.

Je, ni nini hasa kauli ya Serikali kuhusu mbegu hizo ambazo zinaingizwa na hazina ubora nchini na wananchi wanaendelea kupata hasara? (Makofi)

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Noah kwa ufupi tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna Mtanzania ambaye amenunua mbegu na ana receipt ya duka lililomuuzia mbegu ile na mbegu ile ikawa ni fake, atoe taarifa Wizara ya Kilimo, kwa sababu tutamchukulia hatua muuzaji kwa maana ya dealer na distributor.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upo utaratibu wa kisheria ambao unasimamiwa na taasisi yetu ya TOSCI na TOSCI anatoa namba maalum katika kila mbegu inayouzwa mtaani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna Mtanzania amenunua mbegu na ikawa feki tunamkaribisha afike Wizara ya Kilimo, tutachukulia hatua wote. Tunayo kesi Mkoa wa Ruvuma ambayo mtu aliuza mbegu, alizitia rangi na sasa hivi amepelekwa mahakamani, anachukuliwa hatua kwa sababu huu ni uhujumu uchumi na hatuwezi kuruhusu hili. (Makofi)