Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa fidia kwa Wananchi wa Simiyu wanaopakana na Hifadhi za Wanyamapori na kuathiriwa na wanyama hao?

Supplementary Question 1

MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, ahsante napenda kushukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Swali langu ni moja tu la nyogeza. Je, ni lini malipo hayo yataanza kwa sababu yamechukua muda mrefu sana. Ahsante. (Makofi)

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Minza Simon Mjika, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba maombi tayari tumeshayapata na Serikali imeanza kuyahakiki na kabla ya kuisha mwaka huu wa fedha 2022 wananchi hawa watakuwa tayari wameshalipwa.