Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Edwin Enosy Swalle

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupembe

Primary Question

MHE. EDWIN E. SWALLE aliuliza: - Je, lini Serikali italeta muswada wa sheria wa kuweka ukomo wa upelelezi kwenye kesi za mauaji nchini?

Supplementary Question 1

MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwanza nitumie nafasi hii kumshukuru sana Waziri wa Katiba na Sheria na Naibu Waziri, lakini pia nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kupanua wigo wa haki za binadamu nchini Tanzania, nina swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa mwongozo huu ni mwarobaini mzuri wa kusimamia haki za raia wetu nchini. Ni kwa nini mwongozo huu sasa usiingie kama sheria rasmi za nchi yetu? Ahsante.

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Enosy Swalle, Mbunge wa Lupembe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kimsingi wazo lake tunalichukua na tutakwenda kulifanyia kazi kuona tuilete kama sheria au iendelee kusimamia kwenye kanuni hizi. (Makofi)