Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Njalu Daudi Silanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Itilima

Primary Question

MHE. NJALU D. SILANGA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Askari Wanyamapori katika Wilaya ya Itilima na maeneo yanayozunguka Pori la Akiba Maswa?

Supplementary Question 1

MHE. NJALU D. SILANGA: Mheshimiwa Spika, kwanza nawashukuru Wizara kwa majibu mazuri ambayo umeyatoa kulikana na utekelezaji wa kazi waliyoifanya. Nina swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa jukumu kubwa la Wizara ni kuhakikisha wanatoa elimu kwenye maeneo yanayopakana na kandokando ya hifadhi kama vijiji alivyovitaja, lakini kupitia taasisi yake, TAWA aliweza kutoa fedha kwa ajili ya kuanzisha Shule ya Sekondari katika Kijiji cha Nkuyu, Kata ya Nkuyu kwa kushirikiana na wananachi. Sasa Wizara iko tayari kukamilisha ile Sekondari?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Njalu Silanga, Mbunge wa Itilima kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tuliwahi kuweka mradi kwenye shule hiyo aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge na tukajenga madarasa manne; nimwahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaenda kumalizia yale maeneo ambayo yamebaki ili shule hii iweze kufanya kazi.