Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Juma Usonge Hamad

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chaani

Primary Question

MHE. JUMA USONGE HAMAD aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya ukarabati wa Kituo kidogo cha Polisi cha Chaani Lungalunga.?

Supplementary Question 1

MHE. JUMA USONGE HAMAD: Mheshimiwa Spika, nishukuru sana Serikali kwa commitment ya kutaka kukijenga Kituo hicho cha Lungalunga. Sasa naomba niulize swali langu la nyongeza.

Je, ni lini Mheshimiwa Waziri atapanga ziara ya kuja kutembelea kwenye eneo hilo ili wananchi wale wawe na matumaini makubwa kwamba kweli Serikali ina commitment ya kutaka kujenga kituo hiki cha polisi?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Juma Usonge Hamad, Mbunge wa Chaani, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kabla ujenzi wa kituo hicho haujafanyika, nampa ahadi Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakwenda kutembelea eneo hilo tukiwa pamoja naye ili kuweza kujiridhisha kwamba kazi itafanyika. Nashukuru.