Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga uzio na uwanja wa michezo katika Shule Maalum ya Watoto wa kike Asharose migiro iliyopo Wilayani Mwanga?

Supplementary Question 1

MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa Halmashauri ya Mwanga haina mapato ya kutosha, je, Serikali haioni umuhimu wa kuisaidia halmashauri hii ili kujenga uzio katika shule hii muhimu ya wasichana ambayo inapata adha kubwa sana kutokana kutokuwa na uzio, usumbufu, changamoto ya wanyama pamoja na miti kuharibika wakati ambapo ndiyo inaoteshwa? Ahsante sana.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zuena Athuman Bushiri, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeielekeza Halmashauri ya Mwanga na natambua kwamba Mheshimiwa Mbunge anajua, sawa kiwango chao bado sio kizuri sana. Sasa hivi sisi kama Serikali tumekuwa na mipango mingi ikiwemo kumalizia miundombinu ili wanafunzi wetu waweze kukaa katika maeneo salama ambayo yatawasaidia wao waweze kuwa na ufaulu mzuri katika masomo yao. Kwa hiyo, niseme tu kwamba tulipokee kwa mipango ya baadaye ili tuweze kuja kulifanyia kazi baada ya kumaliza hili jukumu la kwanza ambalo tumejipangia kama Serikali.