Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE K.n.y. MHE. KATANI A. KATANI aliuliza: - Je, ni lini mradi wa maji wa Mkwiti utakamilika ili kupunguza tatizo la maji katika Kata ya Mangombya, Mkwiti na Litehu?

Supplementary Question 1

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kimsingi ninachotaka kufahamu ni kwamba mradi huu utakamilika lini? Kwa sababu kumekuwa na tatizo kubwa sana la maji kwenye Wilaya ya Newala, Tandahimba pamoja na Nanyamba hasa zaidi wakati wa kiangazi ambacho ndiyo tunakwenda sasa hivi. Sasa nataka kufahamu ili kuwapa comfort wananchi, mradi huu utakamilika lini ili waweze kupata maji safi, salama na ya kutosha?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cecil Mwambe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika jibu la msingi, nimeeleza kuwa awamu ya tatu na ya nne itakamilika mnamo mwezi Desemba, mwaka huu wa 2022.