Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kurekebisha ramani ya nchi yetu baada ya baadhi ya maeneo kujazwa mchanga kuongeza ukubwa wa ardhi?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize maswali madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, kutokana na mabadiliko ya tabianchi mipaka mingi ya asili baina ya mikoa na mikoa, wilaya na wilaya, kata kwa kata, vijiji kwa vijiji, vitongoji kwa vitongoji imebadilika sana.

Je, Serikali ina mpango gani wa kubadilisha sasa Mipaka hiyo ili iwe sawasawa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali letu la pili. Je, ni nili huo mradi wa Korea utaanza?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaliyoulizwa na Mheshimiwa Ritta Kabati kwa niaba ya Mheshimiwa Angelina Malembeka kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kuhusiana na jambo la tabianchi, ni kweli ipo baadhi ya mito ya asili ambayo imekauka hivyo kusababisha migogoro katika baadhi ya maeneo. Hata hivyo, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pamoja na kulihakikishia Bunge lako kwamba Serikali imeshafanya zoezi la kutambua na kuchora ramani za mikoa hiyo, hivyo suala hilo litakapokuwa limetokea zipo hatua ambazo zimeshachukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, juu ya ni lini mradi utaanza, nataka kulihakikishia Bunge lako kuwa, pale tutakapokuwa tumeshaandaa taratibu zote, ikiwemo kuweka ofisi na kupata wataalam wakaosimamia zoezi hilo, zoezi hilo litaanza.