Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amour Khamis Mbarouk

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbe

Primary Question

MHE. AMOUR KHAMIS MBAROUK aliuliza: - Je, kuna Wavumbuzi wangapi na wa teknolojia gani kwani Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa una lengo la kuchochea uvumbuzi?

Supplementary Question 1

MHE. AMOUR KHAMIS MBAROUK: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kuuliza maswali ya nyongeza, lakini kwanza napenda nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri sana mimi namuombea dua Mwenyezi Mungu amuongezee katika elimu yake hii. Ninayo maswali mawili.

Swali la Kwanza; Serikali inatumia sheria gani kuweka vigezo vya kuwatambua hawa wavumbuzi?

Swali la Pili; amesema kwamba kati ya wavumbuzi waliotambuliwa ni 2,735. Je, katika hawa Zanzibar wapo wangapi? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Amour, Mbunge wa Tumbe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza kwenye majibu yangu ya msingi kwamba Serikali imekuwa ikifanya mchakato wa kuibua hawa wabunifu, wabunifu hawa wanaibuliwa kwa mujibu wa Sheria Na. 7 ya mwaka 1986 ambayo ilianzishwa na Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili kati ya wabunifu hawa 2,735 tumesema wabunifu 376 wanaendelezwa na Serikali, kati ya wabunifu hawa ni wabunifu 11 wanatoka upande wa Zanzibar. Ninakushukuru. (Makofi)