Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. GHATI Z. CHOMETE aliuliza: - Je, ni nini tamko la Serikali kuhusu uchimbaji unaoendelea katika Mto Nyandurumo ambao ni chanzo cha maji kwa wakazi wa Tarime?

Supplementary Question 1

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kuna mradi mpya unaojengwa wa visima kutoa maji Hai kwenda Arusha, lakini kwenye vile vyanzo ambavyo maji yanapita kama kanuni na sheria zinavyotaka kwamba, maeneo ambayo yanaptikana vyanzo vya maji watu wapate. Sasa nauliza swali langu; je, ni lini Serikali itatengeneza miundombinu maeneo ya Hai kwenye mradi mkubwa unaoenda Arusha? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Sera ya Maji inataka maeneo yote ya vyanzo vya maji, wale wanaozunguka makazi yale wananchi wawe wanufaika namba moja. Katika visima hivi anavyoviongelea tayari sisi kama Wizara tuna utaratibu ambao tunaendelea nao, pesa itakapokamilika tutakuja kuendelea kuhakikisha wananchi wote wale wanaokaa kuzunguka vile visima wanaendelea kupatiwa huduma ya maji.