Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, ni lini Ripoti ya Ukaguzi ya Chama cha Msingi Nanjirinji ‘A’ itatolewa ili hatua zichukuliwe kwa wahujumu wa fedha msimu wa 2021/2022?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, shilingi 93,476,190 ni fedha za wakulima wangu wa ufuta 89: Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba fedha hizi zinakwenda kulipwa kwa wakulima hawa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kutokana na changamoto zilizopo katika uendeshaji wa bodi zetu pamoja na vyama vyetu vya msingi na changamoto wanazozipata wakulima kwa uongozi usiokuwa madhubuti, Waziri atakuwa tayari kuambatana nami baada ya Bunge hili kwenda Nanjirinji kuzungumza na wakulima? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ally Mohamed Kassinge, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, la kwanza la kuhusu malipo kwa wakulima, namwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushirika Tanzania kuhakikisha anafuatilia na mwisho wa siku wakulima hawa waweze kulipwa madai yao haya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili kuhusu kuongozana na Mheshimiwa Mbunge, nimwahidi kwamba niko tayari, baada ya vikao hivi vya Bunge tuongozane mimi na yeye kwenda Kilwa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda vizuri. (Makofi)