Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Timotheo Paul Mnzava

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Vijijini

Primary Question

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA K.n.y. MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itajenga bandari kavu eneo la Old Korogwe katika Halmashauri ya Mji Korogwe?

Supplementary Question 1

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru pamoja na majibu ya Serikali naomba kuuliza swali dogo moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kutokana na kazi kubwa sana iliyofanywa na Serikali ya kuboresha bandari ya Tanga na kwa sababu bandari ya Tanga kuwa na eneo dogo, ujenzi wa bandari kavu kwenye eneo la Korogwe ni jambo muhimu sana. Ni lini sasa Serikali itafanya hiyo tathmini ili kuwezesha bandari kavu kwenye eneo la Mji wa Korogwe?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Spika, ahsante napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Kwa sasa Serikali inaboresha na imewekeza sehemu kubwa sana kuboresha bandari ya Tanga ili kuweza kupokea mizigo na kusafirisha mizigo mingi. Kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi tulikuwa bado eneo la Korogwe halijabainishwa kuwa eneo la kujenga bandari kavu, na ndiyo maana Serikali imesema baada ya kupata hilo wazo la Mheshimiwa Mbunge ambaye kazi yake kubwa pia ni kuishauri Serikali tumelichukua na tutafanya tathmini ili tuone kama eneo hilo litafaa kujenga bandari kavu ambayo itakuwa na tija na endelevu, ahsante.