Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. DEUS C. SANGU K.n.y. MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza: - Je, ni lini Serikali itapeleka Boti ya kubebea Wagonjwa katika vijiji zaidi ya saba vilivyopo Mwambao mwa Ziwa Tanganyika katika Jimbo la Nkasi Kusini ambavyo havina huduma ya Zahanati wala Kituo cha Afya?

Supplementary Question 1

MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza kwa niaba ya Mheshimiwa Vicent Paul Mbogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali, lakini nina jambo moja ambalo nataka nimwambie Naibu Waziri; kwamba pesa hizo shilingi milioni 25 zilizotengwa kwa ajili ya ku-repair hizo boti na magari ni kidogo. Kwa sababu hizo boti mbili ziko beyond repair na zimekuwa grounded kwa miaka mitatu. Nataka kujua, Serikali inawaambia nini wananchi wa Jimbo la Nkasi kusini; kwamba itawapelekea lini boti mpya ili waachane na huu mpango wa kutenga shilingi milioni 25 ambazo hazitoshelezi kurekebisha hizo boti? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sangu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa matengenezo ya magari na vifaa mbalimbali katika Halmashauri kwanza ni jukumu la Halmashauri kutenga kwenye bajeti zao; kufanya preventive maintenance ya vifaa pamoja na magari. Ikiwa Halmashauri haina uwezo wa kutosha wa kifedha wa wa kufanya matengenezo makubwa kama hizi boti ambazo ziko beyond repair, wanatakiwa kwanza kufanya tathmini ni kiasi gani cha fedha kinatakiwa kufanya matengenezo yale; na pili, kuomba maombi maalum ya kupata vifaa hivyo kwa ajili ya kutoa huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Mbunge, kwanza wafanye tathmini, hizo boti zinahitaji kiasi gani kufanya matengenezo? Pili, Halmashauri katika vyanzo vyao wana uwezo wa kiasi gani? Kisha wasilishwe sehemu ile inayobaki ili Serikali iweze kuona namna ya kuongeza nguvu kwa ajili ya matengenezo hayo. Ahsante.