Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza: - Je, kwa nini Serikali isiweke utaratibu wa mafunzo ambao utahakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanapangiwa moja kwa moja maeneo ya kwenda kujifunza badala ya utaratibu wa sasa wa mwanafunzi kutafuta mwenyewe?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante na nashukuru kwa majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa nafasi za kufanya mazoezi kwa vitendo kwa wanafunzi bado imekuwa shida sana, inakuwa kama hisani, upendeleo au kujuana kwa mara kadhaa.

Je, ni lini Serikali itaweka muongozo na kanuni ya kuelekeza taasisi za umma na za binafsi na waajiri kuweka utaratibu mzuri wa kuwapokea wanafunzi hawa bila kuhangaika sana? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa vile majibu ya Serikali yameashiria kama hakuna tatizo kubwa kwenye zoezi hili; je, ni kwa nini Serikali isifanye utafiti wa kina wa kubaini changamoto na matatizo yanayowakumba wanafunzi hawa na kuweka utaratibu rahisi wa kupata nafasi? (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba sasa kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asha Abdullah Juma yenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu kwenye programu hizi za mafunzo kwa vitendo na katika programu hizo tunajua kwamba tunapambana au tunakabiliana na changamoto mbalimbali.

Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa changamoto hizi tutaendelea kuzifanyia kazi na kuzitatua, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa vile ametoa ushauri, kwa nini tusifanye utafiti, basi naomba sasa tulichukue wazo hili twende tukafanye utafiti ili kwa pamoja kuweza kukabiliana na changamoto hizi. Nakushukuru. (Makofi)