Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Lucy John Sabu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUCY J. SABU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka Dirisha Maalum la Vijana kwenye kila Benki za Serikali nchini ili kuwawezesha vijana kupata mitaji na mikopo yenye riba nafuu?

Supplementary Question 1

MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Ninalo swali moja dogo la nyongeza; kwa kuwa vijana wengi kutokidhi vigezo na masharti yatolewayo na mabenki.

Je, Serikali haioni haja ya kuweka kigezo cha miradi ama business plan ili vijana wengi waweze kukopesheka? Ahsante.

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Lucy John Sabu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali hilo, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa juhudi zake za kuwatetea vijana. Ni kweli kwamba vijana walio wengi wanamaliza masomo na wengine ni hodari sana, wana uwezo mzuri wa kielimu, lakini hawakopesheki kwa sababu hawana dhamana. Serikali italichukua hili kulipeleka kwa wataalam wetu kulifanyia uhakiki, ikionekana jambo hili linapendeza, basi business plan itatumika kama ni kigezo cha dhamana katika benki za Serikali.