Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Primary Question

MHE. EDWARD O. KISAU aliuliza: - Je, ni lini ahadi iliyotolewa wakati wa kampeni za Urais ya ujenzi wa mabwawa mawili ya maji katika Wilaya ya Kiteto itatekelezwa?

Supplementary Question 1

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na niseme kwa dhati kabisa kwamba nimefurahishwa sana na majibu ya Serikali na wananchi wangu wa Dosidosi, Kijungu na Dongo watakuwa wamesikia haya.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mradi ule wa milioni 400 wa Kaloleni uliotokana na fedha za UVIKO na kwa kweli niishukuru Wizara ya Maji na meneja wa RUWASA aliyeko pale ni mzuri sana, anafanya kazi vizuri sana.

Mheshimiwa Spika, sasa swali langu dogo tu, je, ni lini Wizara ya Maji watakuwa tayari twende Kiteto, hususan pale Dongo, ili tukatembelee mradi mkubwa wa bwawa hili ambalo limewekwa kwenye mpango wa Serikali?Ahsante sana.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Olelekaita kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nimepokea pongezi zote na tuendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa sababu anaendelea kutoa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la kufika Kiteto, niko tayari, nitafika Kiteto na tutafanya kazi. Sisi tunasema na kutenda, tutafika Kiteto.