Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE K.n.y. MHE. KATANI A. KATANI aliuliza: - Je, ni lini Serikali itawalipa wakulima wa Korosho fedha zao walizofanya biashara msimu wa 2017/2018 na iliyokuwa Benki ya Covenant iliyofungwa kabla ya wakulima hawajatoa fedha zao?

Supplementary Question 1

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, majibu ya Serikali ni mazuri kama tulivyosikia, lakini swali: Mpaka sasa kiasi kinacholipwa kutoka kwenye dhamana ni shilingi 1,500,000 tu hata kwa mteja aliyeweka pesa nyingi sana na wanasubiri kuuza mali za benki ndipo waweze kuwalipa; na benki nyingine hazina mali za kutosha.

Je, Serikali haioni kuna haja sasa ya kuleta sheria kwenye Bunge hili ili kuweza kuwasaidia wateja wa benki hizi? Benki ya Greenland, pamoja na benki ya FBME na zenyewe zimefilisika kwa muda mrefu na sasa tunaona Covenant Bank lakini hakuna muda mahususi wa kufanya minada na kuwalipa wateja: -

Je, Serikali na yenyewe haioni kuna haja ya kupanga specific time ili kuweza kuuza mali hizo na ikishindikana Serikali ichukue dhamana hiyo? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Cecil Mwambe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Cecil Mwambe kwa maswali yake haya mazuri, maana yake maswali yake yanaonekana ni mawazo ushauri. Mfano swali la mwanzo, Serikali inalichukua wazo hili na ushauri huu wa kuongeza idadi ya kulipa hiyo fidia ya shilingi milioni moja na nusu kwa wale ambao amana yao iko zaidi ya shilingi milioni moja na nusu.

Mheshimiwa Spika, la pili pia inaonekana ni ushauri kwetu. Kwa hiyo, Serikali itatenga muda mahususi au wakati mahususi wa kukusanya mali na madeni kwa zile Benki ambazo zimefilisiwa na Serikali kwa mujibu wa sheria. Ahsante.