Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Iddi Kassim Iddi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. JAFARI W. CHEGE K.n.y. MHE. ROBERT C. MABOTO Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itasambaza maji katika mitaa ya pembezoni kwa Kata za Kabasa, Guta, Kuzungu, Sazira, Nyatwali, Mcharo na Wariku katika Mji wa Bunda?

Supplementary Question 1

MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Nataka kuiuliza Wizara kwamba ni lini sasa Serikali ina mkakati wa kusambaza maji katika Kata ya Mwaluguru, Kata ya Jana, na Kata ya Ikinda?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, suala la usambazaji maji ni suala ambalo litafanyika mara baada ya kukamilika kwa miundombinu yote kwa sababu lengo ni kuona baada ya uchimbaji wa visima, usambazaji uweze kufuata na akinamama waweze kutuliwa ndoo kichwani.