Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

John Michael Sallu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Vijijini

Primary Question

MHE. JOHN M. SALLU K.n.y. MHE. DUNSTAN L. KITANDULA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kuvipatia maji kutoka mradi wa Mapatano Vijiji vya Kwangena, Bantu na Machimboni Wilayani Mkinga?

Supplementary Question 1

MHE. JOHN M. SALLU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini naomba Serikali ituhakikishie kwamba, katika kipindi hicho cha miezi tisa kweli huu mradi unaweza kumalizika maana tuna shida kubwa sana ya maji pale. Ahsante sana.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kitandula kwa kuwasilishwa na Mheshimiwa John Sallu kwamba, Serikali tumejipanga ndani ya miezi tisa mradi utakamilika na tunaendelea kuongeza nguvu kuhakikisha ikiwezekana kabla ya miezi (9) kufika iwe imekamilika.