Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Norah Waziri Mzeru

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NORA W. MZERU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wafugaji wa Mkoa wa Morogoro kufanya ufugaji wa kisasa na wenye tija kwa kuwa Mkoa huu una wafugaji wengi?

Supplementary Question 1

MHE. NORA W. MZERU: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri kutokana na migogoro ya muda mrefu, baina ya wafugaji na wakulima nchini hususani Mkoa wangu wa Morogoro. Je, Serikali itawasaidiaje wafugaji maeneo ya malisho ili kuepusha migogoro na wakulima? Ahsante. (Makofi)

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nora Waziri Mzeru Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, migogoro ya wakulima na wafugaji katika Mkoa wa Morogoro, tunayo Ranch yetu ya Taifa ya Mkata. Tumekwisha kuanza utaratibu wa kuwagawia wafugaji wenyeji wa Mkoa wa Morogoro. Hadi sasa tumeshatoa vitalu saba, kwa ajili ya wafugaji katika eneo hili na utaratibu huu unaendelea. Pia, Wizara inayo mkakati wa maeneo yake ambayo tumekubaliana kwamba, yako chini ya kiwango cha matumizi ikiwemo baadhi ya Ranch LM News na Holding Grounds. Hizi zote tunazitazama na kuhakikisha kwamba tutazipima na kugawa vitalu baadhi kwa wafugaji walioko maeneo mbalimbali nchini. Ili kuweza kuwasaidia kuondokana na hamahama na kwenda kugombana na wafugaji na wakulima. Ahsante sana.