Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Alice Karungi Kaijage

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kutatua changamoto iliyopo katika vituo vya kutolea huduma za afya ya kukosekana kwa Idara ya Huduma ya Mazoezi Tiba na Utengamao ukilinganisha na ongezeko la wagonjwa wanaohitaji aina hiyo ya tiba?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Namshukuru sana Waziri kwa majibu mazuri, lakini nina swali moja la nyongeza. Kutokana na uhitaji mkubwa na ukuaji wa tatizo hili la stroke, kwa maana ya kupooza na uhitaji wa mazoezi tiba na utengamao: -

Je, Serikali sasa ina mpango gani kuhakikisha kwamba inaboresha vitita vya Bima ya Afya ya Taifa na Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa ili tiba hii iwe jumuishi katika bima hizi kwa ajili ya ustawi wa wananchi wetu? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, kumekuwa na ongezeko kubwa sana la magonjwa yasiyoambukiza ambalo linasababisha uhitaji mkubwa sana wa tiba mazoezi pamoja na huduma za utengemao. Serikali inaendelea kuboresha mpango mkakati ambao utakuja na mbinu; kwanza za kuhakikisha tunaweka mipango madhubuti ya kuzuia magonjwa yasiyoambukiza; pili, kuwa na vifaa tiba vya kutosha na wataalam katika maeneo ya magonjwa yasiyoambukiza na pia utengamao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tutakwenda kuona wazo zuri la Mheshimiwa Mbunge tuone namna gani tunakwenda kuboresha eneo la bima ya afya, lakini na CHF na huduma nyingine kuweza ku-cover huduma hizi za mazoezi tiba na utengamao. Kwa hiyo, tumelichukua wazo hilo, ni zuri sana na kwa kipindi hiki ni wakati muafaka, tutakwenda kuoifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)