Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA K.n.y. MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: - Suala la Vitambulisho vya ujasiriamali limekuwa ni changamoto hasa kwa Wafanyabiashara ambao wana mitaji midogo. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha au kufuta vitambulisho hivyo?

Supplementary Question 1

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza; nataka kujua pesa hizo za vitambulisho ambavyo wajasiriamali wanavitoa huwa zinaingia akaunti gani na mahesabu yake ni yapi, swali la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; wanaonaje wakaweka utaratibu hasa wafanyabiashara wa mbogamboga na mama ntilie ambao mitaji yao ni midogo wakahakikisha kwamba chaji yao inakuwa moja kwa nchi nzima badala ya bei inakuwa juu zaidi kwa sababu wengi mitaji yao ni midogo, ahsante. (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKLI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Sophia Mwakagenda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kwanza ametaka kujua tu fedha za wajasiriamali wadogowadogo zinaingia katika mfuko gani, ni kwamba zinaingia katika Mfuko Mkuu wa Serikali. Kwa hiyo, huko ndiko ambako fedha zinakwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili alikuwa tu anataka kujua ukomo. Nieleze tu kwamba wakati Serikali inapanga ukomo wa shilingi 20,000 ilikuwa imezingatia vipato vya wananchi wetu na ndio maana awali hawa wakina mama ntilie, wafanyabiashara wadogowadogo walikuwa wanalipa fedha nyingi zaidi kwa kuchangia kidogokidogo kila siku lakini ilipowekwa shilingi 20,000 maana yake tulikuwa tumewasaidia kupunguza hiko kiwango. Kwa hiyo, hiki kiwango ambacho kipo kwa sasa bado kinazingatia hali halisi iliyopo lakini sisi tutalipokea ombi lako na tutaendelea kulizingatia kwa kadri ya mahitaji ya wafanyabiashara wetu, ahsante.