Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:- (a) Je, Serikali imejipangaje kukabiliana na wizi wa vyuma unaosababishwa na kushamiri kwa biashara ya chuma chakavu nchini? (b) Je, Serikali haioni kwamba biashara ya vyuma chakavu ni hatarishi hata kwa usalama wa raia na mali zao?

Supplementary Question 1

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwanza nimshukuru Naibu Waziri kwa kunijibu vizuri na Watanzania wamesikia jinsi gani vyuma chakavu vilivyokuwa vinafanya kazi ya kusaidia jamii, lakini hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa suala la vyuma chakavu limekuwa sugu ingawa mazingira wameiwekea kanuni na kwa kuwa suala hili la mazingira limeshamiri la watu kuiba vyuma chakavu kwamba imekuwa kama ni mtaji wao na inaipa taabu Serikali katika kudhibiti ambavyo vyuma kama alivyozungumza Mheshimiwa Waziri.

Je, wako tayari kutuletea sheria itakayokuwa kali inayohusu vyuma chakavu ili tuipitishe hapa Bungeni iweze kusaidia jamii?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa baadhi ya wezi wanaohujumu vyuma chakavu wengi wao wanatumia vilevi ambavyo havikubaliki na jamii ambao kama mfano wanaokula unga, hao ndio jamii kubwa inayofanya kazi hizo za kubeba vyuma chakavu ambavyo vimo katika mitaro ya maji.

Je, suala hili Serikali inalijua na kama inalijua imeliangaliaje…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Fakharia umeshauliza maswali mawili tayari.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, Insha Allah nataka nijue hayo mawili ahsante.

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli sheria zilizopo zinatosha kabisa, lakini ushauri unazingatiwa, kimsingi Mheshimiwa Mbunge tuondoe na tuache tu muhali wale watu ambao wamefanya makosa tuchukue hatua na kuwapeleka sehemu ambayo inayohusika. Ahsante. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naomba kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo ameyaweka mbele ya Bunge lako Tukufu, lakini nimshukuru sana Mheshimiwa Fakharia, ni kweli kabisa wengi kati ya vijana ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli hiyo wamekuwa na dalili zote ambazo zinaviashiria vya matumizi ya dawa za kulevya za aina mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mamlaka ya Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kulevya na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya inachokifanya kwa sasa ni kuanzisha klabu mbalimbali katika mitaa na shule na maeneo mbalimbali kwenye nchi yetu ili kuweza pia kuwabaini hata hao vijana wanaojihusisha na shughuli hizo na shughuli nyingine tu, lakini wanaendelea kutumia dawa za kulevya na lengo letu ni kuwasaidia kuwaondoa huko na kuwaleta katika biashara ambazo hatawajihusisha tena na matumizi ya dawa za kulevya. Kwa hiyo tutaendelea kufanya kazi hiyo nzuri, lengo la Serikali ni kuhakikisha Tanzania bila matumizi na biashara ya dawa za kulevya iwezekane na tuweze kusonga mbele. (Makofi)

Name

Tunza Issa Malapo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza:- (a) Je, Serikali imejipangaje kukabiliana na wizi wa vyuma unaosababishwa na kushamiri kwa biashara ya chuma chakavu nchini? (b) Je, Serikali haioni kwamba biashara ya vyuma chakavu ni hatarishi hata kwa usalama wa raia na mali zao?

Supplementary Question 2

MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri, Serikali imejipangaje kutoa elimu ya namna ya kutenga takataka kulingana na makundi yao kwa sababu kuna zile takataka ambazo zinaoza kwenye mazingira, lakini kuna nyingine kama pastiki na hizo chuma chakavu haziwezi kuoza inabidi zifanyiwe recycling zirejeshwe tena naomba kupata mkakati wa Serikali imejipangaje?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la dada yangu Mheshimiwa Tunza Malapo, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli changamoto ya takataka ambazo zimechanganyika imekuwa ni jambo kubwa sana hata ukienda katika madampo yetu ya kisasa ambayo yanapaswa kutenganisha zile taka unaona kwamba tumekuwa na changamoto kubwa sana katika kupitia hilo ndiyo maana tarehe 3 Juni tuliwaita hapa Maafisa Mazingira wote kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa yote kwa lengo la kuwapa utaratibu mzima jinsi gani wataweza kutoa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na ngazi za mikoa kwa ajenda kubwa kwamba mamlaka hizo zikishirikiana na taasisi yetu ya NEMC ziweze kuhakikisha nchi yetu iko salama.

Kwa hiyo Mheshimiwa Tunza Malapo swali lako ni swali muafaka kabisa na hivi sasa Serikali imeshaliwekea maelekezo na mpango huo unaanza mara moja.