Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itawafanya Wabunge kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi kutokana na ukweli kwamba migogoro mingi ya ardhi na mashamba hupelekewa kesi wao?

Supplementary Question 1

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana; kwa kuwa katika bonde lililoko katika Kijiji cha Nyenza kata ya Mabolilwa kumekuwa kuna mgogoro ambao umechukua miaka mitatu pale kwenye Mabaraza la Ardhi. Sasa kwa kuwa na wananchi wangu wameendelea kusumbuliwa kwenda na kurudi nilikuwa naomba kuuliza swali; je, sheria inampa mamlaka gani Waziri ya kuingilia kati endapo mgogoro umechukua muda mrefu kama huu? Ahsante sana.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria Sura Namba 216 ambayo ndiyo inashughulika na utatuzi wa migogoro, Mheshimiwa Waziri hapaswi kuingilia maamuzi yanayotolewa na vyombo vya utoaji haki. Kama kuna changamoto yoyote ambayo inatokea katika maeneo hayo mlalamikaji anayo nafasi ya kumuona Msajili wa Mabaraza ya Ardhi kuweza kupeleka kero yake na atamsaidia hatua ya kwenda mbele zaidi.