Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anne Kilango Malecela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Same Mashariki

Primary Question

MHE. ANNE K. MALECELA Aliuliza:- Je, Serikali ilishawahi kulifanyia matengenezo yoyote muhimu gari lililotolewa na Mbunge kutoka kwa wafadhili toka Japan na kupelekwa Kituo cha Polisi Gonja katika Jimbo la Same Mashariki mwaka 2015?

Supplementary Question 1

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kupata majibu ya Serikali, lakini sina raha na haya majibu, naomba kuuliza maswali mawili.

Kwa kuwa wakati wa Bunge la Kumi nilishauliza hili swali mara mbili, kwa sababu hili gari limekuwa bovu kwa muda mrefu; je, Serikali mnavyonijibu leo mko serious kweli hili gari litatengenezwa na litatengenezwa lini?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, hivi Serikali inafahamu kwamba hiki Kituo cha Polisi kipo Mahore na Mahore ni tambarare na asilimia 68 ya wananchi wa Jimbo la Same Mashariki wanaishi milimani na kama kituo kile kinakuwa hakina gari wale wananchi hawana ulinzi na maisha yao.

Je, Serikali mnalijua hilo na kama mnalijua mtafanya jitihada ya kutengeneza hili gari? Ahsante.

Name

George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Same Mashariki kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa kwamba gari hili ni bovu na ni kweli kwamba ni muda mrefu, lakini ni ukweli pia ambao Mheshimiwa Mbunge hajausema. Gari hili alipewa baada ya yeye kutoa gari kwa Jeshi la Polisi aliyekuwa amepewa msaada na wafadhili wake, kwa ajili ya kituo hiki. Sasa kwa sababu gari lile aliyekuwa la kwake aliyekuwa amepewa lilikuwa la kisasa sana ambalo kwa kweli lisingeweza kupelekwa kule kijijini, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi walilibakiza kwa ajili ya shughuli za Makao Makuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa leo hii Mbunge anaposikitika hivi mbele yako niseme tu kwa niaba ya Serikali na Wizara tutaitengeneza hili gari mapema iwezekanavyo ili kutoa heshima na shukrani kwa Mheshimiwa Mbunge, lakini kwa nia njema tu ya kufanya ndugu zetu wale wa Same Mashariki, kule Mahore wapate huduma hii vizuri zaidi. Nakushukuru sana. (Makofi)