Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Primary Question

MHE. DAVID E. SILINDE aliuliza:- Nchi Wahisani na Wa shirika wa Maendeleo wamekuwa wakishindwa kuleta misaada na ahadi zao kwenye utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo kwa wakati na nyakati nyingine kushindwa kuleta kabisa katika kipindi cha miaka mitatu ya fedha mfululizo iliyopita ya 2016/2017, 2017/ 2018 na 2018/2019:- Je, Serikali inatueleza ni kitu gani kinasababisha hali hii?

Supplementary Question 1

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya ngongeza.

(a) Ni kwa nini sasa fedha za Wahisani zinachelewa kufika kwa wakati na nyingi zinakuja wakati tunamaliza mwaka wa fedha?

(b) Naomba sasa Serikali itoe orodha ya nchi wahisani ikionesha mwenendo wa walichochangia katika kipindi cha miaka mitatu ya fedha iliyopita?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa David Ernest Silinde, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, Washirika wa Maendeleo hutoa fedha kulingana na makubaliano ya kimkataba yaliyopo kati ya Serikali na washirika hao. Kwa kutambua hilo, baadhi ya Washirika wa Maendeleo hutoa fedha mwishoni mwa mwaka wa fedha wa Serikali kutokana na kupishana kwa kalenda kati ya mwaka wa fedha wa Serikali na kalenda za mwaka wa fedha wa Washirika wa Maendeleo, jambo ambalo Serikali hulizingatia katika mipango yake.

Hivyo basi, siyo kweli kwamba fedha za wahisani zinachelewa kufika kwa wakati. Fedha hizo hutolewa kwa mujibu wa mikataba hiyo ambayo inaainisha muda ambao Washirika wa Maendeleo wanatakiwa kutoa fedha hizo ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopangwa kutekelezwa na Serikali.

(b) Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita (2016/2017 – 2018/2019), Serikali imekuwa ikipokea fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kutoka kwa nchi wahisani kwa kiwango cha kuridhisha kutoka kwa nchi wahisani pamoja na Washirika wa Maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Umoja wa Ulaya, Japan, Korea, India, Finland, Ufaransa, Ujeruman, Global Fund, IFAD, Norway, Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na Sweden.

Aidha, orodha ya nchi wahisani pamoja na Washirika wa Maendeleo ikionesha mwenendo na kiasi walichochangia kwa kipindi hicho tutaiwasilisha kwa Mheshimiwa Mbunge baada ya kufanya uchambuzi wa kina kama alivyoomba.