Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Wananchi wa Jimbo la Same Mashariki wako tayari kuanzisha misitu ya vijiji kwenye maeneo yenye ukame kama vile Kata za Bendera, Kihurio, Ndugu na Maore ili kuhifadhi mazingira. Je, Serikali ipo tayari kuanzisha miradi ya utunzaji wa mazingira katika kata tajwa kwa kufundhisha wanavijiji uanzishwaji wa misitu ya vijiji?

Supplementary Question 1

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kweli jibu limekuwa la ujumla sana nipende tu kusema kwamba Kata za Bendera, Ndungu, Kihurio zina ukame mkubwa sana na hata hivi tunavyoongea hakuna hata msitu mmoja ni Kata ya Maore tu ambayo ina kamsitu kadogo kaasili.

Swali langu la pili ni je, Serikali iko tayari kusaidiana na wanavijiji kutenga maeneo kisheria ambayo yatakuwa ni misitu ya vijiji badala ya kusema halmashauri inafanya wakati hatuoni kwamba sehemu hizi zinatendewa haki kwa kuotesha miti ambayo itapunguza ueneo wa jangwa katika eneo hili? Ahsante.

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi kwamba zoezi hili limekuwepo la uhamasishaji wa upandaji miti na Wizara yangu ina mkakati wa katika mwaka 2016 – 2021 kupanda miti milioni mia mbili na themanini katika maeneo mbalimbali ya nchi. Tumechukua mapendekezo ya Mheshimiwa Mbunge kwenda katika eneo husika kwa kushirikiana na Serikali za vijiji ili vijiji vyenyewe vitoe ridhaa ya maeneo ambayo vinataka tuyatenge na kuyachukua na kuyaboresha kwa ajili ya misitu hiyo lakini uzoefu unaonesha sehemu nyingi ambazo tumekwenda baada ya kuyachukua maeneo haya na kuyaboresha wanavijiji tena wamerudi na kuyadai maeneo haya waweze kurejeshewa. Kwa hiyo, kama Mheshimiwa Mbunge yuko tayari kutoa ushirikiano Wizara yangu itakuwa tayari kutoa ushirikiano huo wa kwenda kuhamasisha upandaji miti katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, lakini katika swali lake la pili tutatuma wataalam wetu katika Wizara yetu kwenda kuangalia uwezekano wa kuanzisha vitalu vya miti katika Kata hizo alizozitaja Mheshimiwa Mbunge.