Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maryam Salum Msabaha

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA aliuliza:- Kuna baadhi ya Bar na Club ambazo zimejengwa kwenye makazi ya watu ambazo zimekuwa kero kwa jamii:- Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusu Bar na Club hizo ambazo zinakiuka sheria na maadili ya jamii?

Supplementary Question 1

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Spika, ahsante, nianze na hapa kwenye huu Mkoa wako wa Dodoma. Niko maeneo ya katikati hapo Mjini, baa hizi zimekuwa kero kwa wananchi ambao wamejenga maeneo karibu na hizi bar.

Mheshimiwa Spika, isitoshe, wamekuwa wanatoka wanawake mbalimbali, wengine wanatoka Dar es Salaam, wanatoka Morogoro, wanatoka mikoa mbalimbali wanakuja hapa kwenye Jiji hili la Dodoma kwa sababu ni Makao Makuu ya Serikali. Tatizo kubwa bar hizi zinapiga miziki na matusi makubwa sana kwa jamii, imekuwa ni kero kubwa sana kwa jamii.

Je, ni lini Serikali itahakikisha inafanya msako maalum kwa Mkoa huu wa Dodoma, hasa ukichangia maeneo ya Mjini niliyoyataja Mheshimiwa Waziri?

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuna hawa akinamama ambao hawataki kufanya kazi wanajiingiza kwenye haya masuala yasiyokuwa ya stahiki za kijamii yaani kama tukisema kama Marekani wao wana tozwa kodi, Uholanzi wanatozwa kodi, sasa hawa wanawake askari wa Dodoma wamekuwa mara kwa mara askari kanzu wamekuwa wakiwachukua mara kwa mara lakini wanarudi tena kwenye maeneo haya haya wanakuwa wanafanya matukio ambayo hayaendani na jamii ya Kitanzania na maadili.

Je, Serikali ina mikakati gani kuhakikisha inawachukua wanawake wote hawa ambao wanafanya biashara haramu ambazo hazina stahiki na kuangalia hata wanawapeleka kwenye mashamba ya JKT wakafanye kazi? Naomba jibu la Serikali.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maryam Msabaha, meti wangu wa kambi yetu ya Bulombola kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kilio hiki cha Dodoma kikubwa zaidi nini mkakati wa Serikali? Nimuelekeze Mkuu wa Mkoa kwa sababu akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa, na Mkuu wake wa Wilaya kuhakikisha kwamba vile vitendo vya hovyo vyote ambavyo vinakiuka utaratibu waweze kuvisimamia kwa sababu Jeshi la Polisi hapa lipo waangalie nini kinachofanyika kuhakikisha hadhi ya Jiji la Dodoma linabakia kama lilivyo badala ya kuchafuliwa.

Mheshimiwa Spika, mkakati hawa watu ambao hii kauli nyingine uliyoizungumza ya watu inawezekana wanafanya biashara zisizo sawasawa, ndiyo maana Serikali mnakumbuka mwaka jana hapa tulipitisha sheria asilimia 10 iende katika vikundi ya vijana, akinamama na walemavu. Imani yetu ni kwamba kwa vile ukiangalia Dodoma pato lao ni kubwa mpaka juzi juzi wamekusanya zaidi ya shilingi bilioni 55 own source collection. Kwa hiyo ukichukua hapo asilimia nne yake maana yake ni fedha nyingi sana, kwa hiyo vikundi hivi ninaimani kwamba viongozi wetu watendaji wetu hasa maafisa maendeleo ya jamii chini ya Mkurugenzi wakiweka utaratibu mzuri wa kuwawezesha hawa akinamama tutawatoa katika suala zima hatarishi walilokuwepo nalo kwa wao kwamba kujiingiza katika shughuli halali za kiuchumi za Taifa letu hili.

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA aliuliza:- Kuna baadhi ya Bar na Club ambazo zimejengwa kwenye makazi ya watu ambazo zimekuwa kero kwa jamii:- Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusu Bar na Club hizo ambazo zinakiuka sheria na maadili ya jamii?

Supplementary Question 2

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwenye awamu ya tatu nyumba za Serikali ziliuzwa na nyingi zilikuwa zile za Shanti Town kule Moshi, Oysterbay Dar es Salaam, Gangilonga na Wilolasi Iringa na hapa Kilimani Dodoma na kwingineko. Nyumba hizo zilikuwa ni za makazi na zilikuwa ni eneo tulivu sana zikiitwa uzunguni. Lakini nyumba hizo ndiyo zimegeuka sasa ni Bar, ni maeneo ya kuoshea magari kule Moshi Shanti town zinasumbua wananchi na watoto hawalali. Ni lini sasa Serikali italeta sheria hapa Bungeni kama zile sheria za awali hazifuatwi ili zikatazwe kabisa?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, ni kweli hii ni kero kubwa sana mpaka hivi leo asubuhi nilikuwa naongea na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwamba ukiangalia kuna jengo la sinema karibu ya Shule ya Sekondari ya Arusha Girls na Shule ya Sekondari nyingine katikati, inaonekana badala ya kuweka jengo la sinema la kawaida sasa imekuwa sehemu ya night club na mambo vuruguvurugu hata hivyo kuhatarisha hasa madhara makubwa kwa wanafunzi wetu.

Mheshimiwa Spika, lakini maeneo hayo uliyoyazungumza ni kweli mkakati wa Serikali nadhani sheria ipo isipokuwa ni enforcement ya hizi sheria tu ndiyo inatakiwa. Kikubwa zaidi niwaelekeze viongozi wetu katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa ambao ni Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya palepale ninaimani wakizingatia vizuri eneo hili la kusema kuleta utulivu katika maeneo yao ninaamini kwamba jambo hili halitokuwa na mashaka. Kwa hiyo, niwaagize wakuu wa mikoa wote sasa waanze kufanya ufuatiliaji wa karibu kukomesha vitendo hivi vya hovyo vinavyotokea katika mazingira yetu ambao siyo jambo jema katika Taifa letu.

Name

Joseph Roman Selasini

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Rombo

Primary Question

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA aliuliza:- Kuna baadhi ya Bar na Club ambazo zimejengwa kwenye makazi ya watu ambazo zimekuwa kero kwa jamii:- Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusu Bar na Club hizo ambazo zinakiuka sheria na maadili ya jamii?

Supplementary Question 3

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru hizi bar zinamilikiwa na watu wakubwa sana na wenye fedha hata miongoni mwetu vilevile kuna baadhi ambao tuna hizi bar, na ni kutokana na mipango miji kutozingatiwa. Sasa ni kwanini Serikali isitoe tu tamko kwamba kuanzia sasa bar hizi zinazojengwa hovyo hovyo ni marufuku na atakayetoa kibali hatua zitachukuliwa?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema na Mheshimiwa Mbunge amesema wamiliki wa hizo bar wengine ni wakubwa inawezekana wengine wako humu ndani, kikubwa zaidi sheria ipo. Jambo kubwa linalotakiwa kufanywa sasa hivi ni kufanya usimamizi wa sheria, ndiyo maana hapa nimezungumza siwezi kutoa matamko tu hivi hivi kwa sababu sheria tayari ipo ni lazima tuzingatie tunasema STK – Sheria, Taratibu na Kanuni.

Mheshimiwa Spika, nina imani viongozi wangu wote wa ngazi za chini huko chini hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya naomba wawe wakali hasa kuona haya mambo yasiyokuwa sawasawa wayasimamie kuondoa hii kero ambayo Mheshimiwa Selasini hapa ameizungumza.