Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 33 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 273 2019-05-22

Name

Maryam Salum Msabaha

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA aliuliza:-

Kuna baadhi ya Bar na Club ambazo zimejengwa kwenye makazi ya watu ambazo zimekuwa kero kwa jamii:-

Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusu Bar na Club hizo ambazo zinakiuka sheria na maadili ya jamii?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba biashara nyingi, zikiwemo za uendeshaji wa bar na club zipo kwenye maeneo ya makazi ya watu. Serikali inawaelekeza wamiliki wote wa bar na club kuwa wanapaswa kuzingatia maelekezo ya Sheria ya Vileo Sura Na. 28 ya mwaka 1968, kifungu cha 14(1) katika uendeshaji wa shughuli zao. Aidha, Serikali haitasita kuchukua hatua kwa vitendo vyovyote vitakavyobainika kukiuka sheria na kusababisha kero kwa wananchi wengine.