Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Mohamed Chuachua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Primary Question

MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA aliuliza:- Jimbo la Masasi lina Shule moja tu ya Sekondari ya Kidato cha Tano na Kidato cha Sita ambayo ni ya Kitaifa ingawa mahitaji ya Wanafunzi wanaofaulu kwenda Kidato cha Tano na Kidato cha Sita yameongezeka sana, Shule pekee ya Kidato cha Tano na Kidato cha Sita iliyopo Masasi ni Shule ya Sekondari ya Wasichana Masasi:- (a) Je, ni lini Serikali itazipandisha hadhi Shule za Sekondari za Mwenge Mtapika na Anna Abdallah ili ziweze kupokea Wanafunzi wa Kidato cha 5 na 6; (b) Jimbo la Masasi linahitaji vyumba 27 vya maabara ambapo hadi sasa vyumba Saba tu ndiyo vina vifaa vya maabara katika shule Nne; Je, ni lini Serikali itapeleka vifaa vya maabara katika Shule zote za Sekondari? (c) Ikama ya Walimu wa Sayansi katika shule za Sekondari Tisa zilizopo Jimbo la Masasi ni Walimu 84 japokuwa waliopo ni 24 tu; Je, Serikali inaweza kulifanya jambo hili kama dharura inayohitaji utatuzi wa haraka kwa kutuletea Walimu 60 wa Sayansi?

Supplementary Question 1

MHE.DKT. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwa sasa kuna upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi katika Halmashauri ya Masasi na walimu 46 wanahitajika ili kukidhi Ikama ya walimu wa masomo ya sayansi;

Je, ni lini Serikali italeta Walimu hao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kwamba kwa kuwa suala la kukosekana kwa walimu wa sayansi ni suala la Kitaifa, na kwa kuwa wanafunzi wengi wanaomaliza kidato cha nne na kidato cha sita hawachagui kwenda kujiunga na masomo ya ualimu wa masomo ya sayansi, hivi Serikali haioni kunatakiwa kuwe na jitihada za maksudi za kuchochea watoto hawa ili waweze kujiunga na masomo ya ualimu wa sayansi hususan kwa kuondoa ama kupunguza ada kwa masomo ya Diplomaya Ualimu wa Sayansi na Degree ya Ualimu wa Sayansi?

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kuendelea kufuatilia suala la elimu hasa katika masomo ya sayansi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anataka kujua ni lini walimu wa sayansi watapelekwa katika maeneo haya. Ni kweli kwamba kuna upungufu wa walimu wa sayansi na hisabati katika shule zetu za sekondari lakini tumepata kibali mwaka wa fedha uliopita tukaajiri walimu 4,500 na sasa tunasubiria kibali kingine takribani walimu 15,000. Tukipatakibali hicho tutaajiri, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge maeneo yote ambayo yana upungufu tutaanza nayo, pale palipo na upungufu mkubwa tunaanza na kuendelea katika maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nia ya Serikali ni kuwa na walimu wa kutosha katika masomo ya sayansi ili kuweza kuboresha elimu hii ya sayansi hasa kwenye dhana nzimainayohusiana na Serikali ya Awamu ya Tano ya sera ya maendeleo ya viwanda na uchumi endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anazungumzia kama kuna uwezekano wa kupunguza ada katika masomo na hasa katika Diplomaili wanafunzi wengi na vijana wengi wajiunge katika masomo ya sayansi na hasa Ualimu ili waweze kupunguza changamoto hii. Kwanza gharama inayotumika sasa siyo kubwa ni gharama ya kawaida kabisa na Serikali imejitahidi sana kupunguza michango mingi ambayo ilikuwa inafanyika. Sasa hivi tumeshapeleka vijana wengi katika Vyuo hivi, wataendelea kusoma na ada ni ya kawaida. Ahsante.(Makofi)

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Primary Question

MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA aliuliza:- Jimbo la Masasi lina Shule moja tu ya Sekondari ya Kidato cha Tano na Kidato cha Sita ambayo ni ya Kitaifa ingawa mahitaji ya Wanafunzi wanaofaulu kwenda Kidato cha Tano na Kidato cha Sita yameongezeka sana, Shule pekee ya Kidato cha Tano na Kidato cha Sita iliyopo Masasi ni Shule ya Sekondari ya Wasichana Masasi:- (a) Je, ni lini Serikali itazipandisha hadhi Shule za Sekondari za Mwenge Mtapika na Anna Abdallah ili ziweze kupokea Wanafunzi wa Kidato cha 5 na 6; (b) Jimbo la Masasi linahitaji vyumba 27 vya maabara ambapo hadi sasa vyumba Saba tu ndiyo vina vifaa vya maabara katika shule Nne; Je, ni lini Serikali itapeleka vifaa vya maabara katika Shule zote za Sekondari? (c) Ikama ya Walimu wa Sayansi katika shule za Sekondari Tisa zilizopo Jimbo la Masasi ni Walimu 84 japokuwa waliopo ni 24 tu; Je, Serikali inaweza kulifanya jambo hili kama dharura inayohitaji utatuzi wa haraka kwa kutuletea Walimu 60 wa Sayansi?

Supplementary Question 2

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Mtama lina shule za sekondari mbili ambazo zinapokea vijana waKidato cha Tano na Kidato cha Sita. Shule ya Sekondari Nyangao na Shule ya Sekondari Mahiwa. Mwaka jana Naibu Waziri wa Elimu alipotembelea Jimboni Mtama alipoenda kuiona Shule ya Sekondari Mahiwa alikuta majengo yake yamechoka na yamekuwa ya muda mrefu na akaahidi kwamba Serikali itatoa fedha kusaidia ukarabati wa majengo hayo.

Je, Serikali iko tayari kutekeleza ahadi yake kwa wananchi wa Jimbo la Mtama?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba nilitembelea Jimbo la Mheshimiwa Nape na ni kweli kwamba alinisihi nimsaidie shule yake iweze kupata miundombinu ili iweze kuwa bora na hatimaye kuwa shule ya Kidato cha Tano na Kidato cha Sita. Naomba niendelee kumuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imepanga kupeleka fedha katika Awamu ya Nane ya Mpango waEP4R, kwa hiyo, ahadi yetu iko palepale na itatekelezwa.(Makofi)