Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Mohamed Chuachua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Primary Question

MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA aliuliza:- Mkoa wa Mtwara una jumla ya Vijiji 869 na Vitongoji 1,826 na jumla ya Vijiji 372 vimethibitishwa kupatiwa umeme ikijumuishwa kufanya Vijiji vitakavyosalia kuwa 497 na hii ni sawa na wastani wa 23.6% ya utekelezaji wa huduma kwa kila Wilaya ndani ya Mkoa. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza miradi ya REA katika mkoa huu? (b) Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya Mji wa Masasi ilitengewa Vijiji saba tu kati ya Vijiji 31, je, ni lini vijiji vilivyobaki vitapatiwa umeme?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza kwa kuwa mpango ulikuwa ni kupeleka umeme katika vijiji saba na mkandarasi kwa sasa hayuko site isipokuwa kwenye kijiji kimoja ambacho amepeleka umeme kwenye kaya saba peke yake.

Mheshimiwa Spika, kwa nini Serikali haioni haja ya kumfukuza mkandarasi huyu ambaye hafanyi kazi kwa kasi inayohitajika kwa kuwa site hayupo na kwa sababu ni vijiji vichache sana ambavyo vimewekewa umeme na pia alipewa vijiji vichache?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, tumeambiwa Mji wa Masasi umeungwa na Grid ya Taifa kutokea Mkoa wa Ruvuma lakini hali ya kukatikakatika kwa umeme ni mbaya zaidi kuliko hata kabla haijaungwa. Ni juhudi gani sasa zinatakiwa zifanywe na Serikali kuhakikisha kwamba inawaondoa wananchi wa Masasi katika adha hii kubwa nay a muda mrefu ya kukatikakatika kwa umeme? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Chuachua, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mkandarasi ambaye yuko site, kwanza tunataka atimize wajibu wake kwa mujibu wa mkataba aliousaini. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, suala hilo litafuatiliwa ili kujua tatizo lake ni uwezo au ni jambo gani ili aweze kuchukuliwa hatua zinazostahili.

Mheshimiwa Spika, kwa sehemu ya pili, niseme tu kwamba kwa ufahamu nilionao ni kwamba kwa sasa bado Masasi haijaungwa kutoka kwenye Gridi ya Taifa kutoka Mkoa wa Ruvuma kwa sababu hata hiyo line haijajengwa isipokuwa kuna mpango wa kufanya hivyo. Naamini endapo utekelezaji huo utafanyika, hali ya Mji wa Masasi itakuwa ni bora zaidi ikizingatiwa kwamba umeme ambao umekuja mpaka Songea Mjini Ruvuma ni wa KV 220 na capacity ya megawatt 60 ni mwingi na unatosheleza kupeleka mpaka maeneo hayo.

Name

Hawa Abdulrahiman Ghasia

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. RASHID M. CHUACHUA aliuliza:- Mkoa wa Mtwara una jumla ya Vijiji 869 na Vitongoji 1,826 na jumla ya Vijiji 372 vimethibitishwa kupatiwa umeme ikijumuishwa kufanya Vijiji vitakavyosalia kuwa 497 na hii ni sawa na wastani wa 23.6% ya utekelezaji wa huduma kwa kila Wilaya ndani ya Mkoa. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza miradi ya REA katika mkoa huu? (b) Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri ya Mji wa Masasi ilitengewa Vijiji saba tu kati ya Vijiji 31, je, ni lini vijiji vilivyobaki vitapatiwa umeme?

Supplementary Question 2

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nami napenda kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, katika Halmashauri yangu ya Mtwara Vijijini ninazo kata mbili za Moma na Muungano ambazo mpaka sasa hivi mkandarasi hajaweka umeme hata kijiji kimoja. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba anawapelekea wananchi hao umeme kwa haraka?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hawa Ghasia, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika masuala ya kuweka umeme kuna hatua. Hatua ya kwanza ni mipango kama kawaida na ku-plan network kama itakavyokuwa. Hatua ya pili ni ya kujenga kwa mfano kujenga line kubwa au line ndogondogo na baada ya hapo kuweka transforma na kuwasha. Katika misingi hiyo niseme tu kwamba nalichukua kama ambavyo umeeleza kumfuatilia huyo mkandarasi tuone kwamba hajafanya kitu kabisa au yuko kwenye hatua ambazo zimebakiza kuweka transforma tu na kuwasha.

Mheshimiwa Spika, natoa rai kwa wakandarasi wote nchini kwamba suala la umeme katika vijiji kama ambavyo Serikali inategemea kusambaza umeme katika vijiji vyote Tanzania ni la muhimu hasa ikizingatiwa katika kipindi hiki ambacho Watanzania wanahitaji kuwekeza katika viwanda na shughuli mbalimbali za kibiashara na maisha yao.

Kwa hiyo, niwaombe wakandarasi, Serikali imewapa heshima, hasa wakandarasi wa ndani kuwapa nafasi ya kufanya kazi hizo badala ya kuwategemea wakandarasi wakubwa kutoka nje, watumie wakati huo mzuri na watumie nafasi hiyo kuhakikisha kwamba hawaiudhi Serikali na kusababisha kuwanyang‟anya kazi na kuwapa kazi wakandarasi kutoka nje jambo ambalo walikuwa wakililalamikia siku zote.