Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza:- Kuna harufu mbaya inayotoka kwenye chumba cha Mahabusu katika Kituo cha Polisi Mazizini Zanzibar na kuwa kero kwa Askari na wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo. Je, ni lini Serikali itakifanyia ukarabati kituo hicho ili kuondoa harufu hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali na napongeza juhudi kubwa za Serikali kwa kujenga Kituo kipya huko Chukwani.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, Chukwani ni nyuma kidogo, Mazizini ni barabarani na ni centre na karibu na Shehia nyingi kama vile Shakani, Kombeni, Maungani na kadhalika. Sasa kile Kituo cha Wilaya kwa nini hiki cha Mazizini mnataka kukiua?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, kwa nini msifanye taratibu kama hivyo mnavyoshirikiana na wadau kufanya kampeni ya kuboresha vyoo na vyumba vya mahabusu kwa nchi zima mkianzia na hapo Mazizini?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, hatutarajii kukiua Kituo cha Mazizini, kitu ambacho tunafanya ni kuhamisha kuwa Kituo cha Wilaya, kuhamishia Chukwani. Kwa hiyo Kituo cha Mazizini kitaendelea kutumika tu, tutafanya jitahada ya kukikarabati na kwa kuwa kiko barabarani kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema, tunaamini kwamba kinahitajika kuendelea kutoa kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, kuhusu ukarabati wa vituo vyetu kwa ujumla wake ikiwemo mahabusu, ni jambo ambalo tunakwenda nalo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wake kuhusu kuwatumia wadau ndiyo tumekuwa tukiufanya kazi, wako wadau ambao wamekuwa wakishirikiana nasi kwa dhamira ya kurekebisha mazingira ya Vituo vyetu vya Polisi ikiwemo mahabusu.