Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prosper Joseph Mbena

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. PROSPER J. MBENA aliuliza:- Vigezo vilivyotumika kuchagua Vituo vya Afya 100 kupatiwa shilingi milioni 700 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara na upasuaji wa akina mama wanaojifungua kwa maana ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya maabara na upasuaji na shilingi milioni3 00 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa toka MSD ni vigezo ambavyo pia vipo katika Vituo vya Afya Duthumi, Tawa, Mvula na Mtamba katika Jimbo la Morogoo Kusini. Je, ni lini Seikali itawatendea haki wananchi wa Morogoro Kusini kwa kuwatengea fedha ili kukamilisha miundombinu ya upasuaji angalau kituo kimoja Kata ya Duthumi, Tawala Mvuha na Mtamba?

Supplementary Question 1

MHE. PROSPER J. MBENA: Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru Serikali kwa msaada huo katika sehemu hizo mbili zilizotajwa naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Je, ni lini Serikali itazisaidia Vituo vya Afya vya Mtamba pamoja na Kisaki ambavyo mchakato wake Serikali ulishaanza kushughulikia?

Je, ni lini Serikali itapeleka au itasaidia Hospitali Kuu ya Mkoa wa Morogoro mashine ya CT-Scan ili kuokoa maisha ya watu ambao yanapotea bure kwa ajili ya kukosa huduma ya mashine hiyo?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimetaja katika jibu la msingi Wilaya ya Morogoro Vijijini ambayo Mheshimiwa anatoka ni miongoni mwa Wilaya ambazo zimepata nafasi ya kujengewa Hospitali za Wilaya na tumeanza kupeleka shilingi bilioni 1.5 lakini ili ikamilike tunahitaji tunahitaji jumla ya shilingi bnilioni 7.5. Lakini mwenyewe anakiri kwamba tayari tumeanza kujenga Kituo cha Afya pale Duthumi, najua kabisa kiu ya Mheshimiwa Mbunge kwamba na maeneo mengine Vituo vya Afya vijengwe naomba nimuakikishie kwamba ni azima ya Serikali kwa kadri bajeti inavyoruhusu tumeanza na vituo 350 lakini azma kuhakikisha kwamba katika kata zetu zote kwa kadri bajeti itakavyo kuwa inaruhusu kama ambavyo tumeahidi kwenye ilani ya CCM tunaenda kutekeleza.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa mwongozo wetu wa Wizara ya Afya huduma za CT-Scan zinapatikana kuanzia Hospitali za ngazi ya Rufaa za Kanda. Lakini baada ya kuwa tunafanya mapitio katika hii sera mpya tunajaribu kuangalia huduma sasa hivi katika nchi yetu zimekuwa sana na tumeona kwamba baadhi ya hospitali za mikoa ambazo ziko kimkakati. Lakini vilevile huduma hizi za CT-Scan zinahitaji utaalamu wa hali ya juu kuweza kuzitumia ambazo zingine huduma hizi hazipatikani katika Hospitali za Mikoa, Hospitali Wilaya na kushuka chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mkakati wetu sisi kama Serikali nikujaribu ku-identity mikoa ile ambayo ni ya kimkakati ikiwa ni pamoja na Morogoro kwa sababu kuna aya inapita pale ili huduma hizi ziweze kupatikana kwa lengo kuhakikisha kwamba tunazuia ajali baadhi ya Mikoa lakini hatutaweza kuzishusha huduma chini ya ngazi ya hospitali ya rufaa Mikoa kwa sasa.