Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hamida Mohamedi Abdallah

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Lindi Mjini

Primary Question

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH aliuliza:- Kilwa ni moja ya miji mikongwe katika Afrika Mashariki tangu Anno Domino (AD) 900 -1700 pamoja na miji mingine ya Lamu, Mombasa, Sofala na Zanzibar. Miji hiyo ilipewa heshima ya jina la Urithi wa Dunia (World Heritage Site). Kwa kawaida miji hiyo husaidiwa na Mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani, Japan, Ujerumani, Uingereza na Shirika la UNESCO:- Je, Serikali ya Tanzania imefaidika nini kutoka katika Mataifa hayo yanayosaidia nchi za urithi wa dunia?

Supplementary Question 1

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH. Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu haya ya Serikali. Swali la kwanza, maeneo haya ni yale ambayo walikaa wakoloni wa mataifa haya makubwa ambayo leo hii wanasaidia. Je, Serikali imesaidia kwa namna gani katika kuendeleza miundombinu ya Kilwa Kisiwani na Msongo Mnara ili kuendeleza utalii wa maeneo haya? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili la nyongeza, napenda kujua Serikali inasaidiaje katika kuhakikisha Kilwa Kisiwani na Msongo Mnara tunaendeleza utalii, maana hali ya kule ni mbaya sana, miundombinu ni mibovu, watalii sasa wanapungua kwa sababu hakuna hoteli, hakuna vifaa vya kuwawezesha watalii kuvuka kwenda Kilwa Kisiwani na Kilwa Msongo kuona haya magofu ya ukoloni? Ahsante sana.

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Hamida Abdallah, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nachukua nafasi hii kutambua mchango wake ambao amekuwa akiutoa katika hii sekta ya utalii kule Lindi. Kwa kweli amekuwa akifanya kazi nzuri sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa katika lile eneo mimi mwenyewe nimefika Machi na nimeona jinsi miundombinu ambavyo iko kwenye hali mbaya. Hiyo inasababisha watalii wengi washindwe kufika katika lile eneo. Hivi sasa tumeandaa mkakati maalum kwa ajili ya kuboresha ile miundombinu katika vile Visiwa vya Kilwa pamoja na Songo Mnara ili kuhakikisha ile miundombinu inapitika wakati wowote; iwe ni kipindi cha masika au kipindi cha kiangazi, kusudi watalii waweze kufika.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya changamoto kubwa ambayo iko pale ni pamoja na kutafuta boti ya kisasa itakayokuwa inawavusha watalii kuwapeleka kule katika Kisiwa. Sasa hili tunashirikiana na Wizara ya Uchukuzi ili tuone namna ambavyo tunaweza tukapata boti nzuri ya kuweza kusaidia katika shughuli hizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kuhusu namna ya kuimarisha utalii katika eneo lile, mpango mkubwa ambao tunao kama Wizara ni pamoja na kuunganisha na Pori la Akiba la Selous. Tunataka iwe ni circuit moja, watalii wanapokwenda kutembelea Selous katika upande ule, basi tuunganishe na hii circuit ya Kilwa Kisiwani pamoja na Songo Mnara kusudi vyote kwa pamoja iwe package moja. Hiyo tunaamini itasaidia sana katika kuimarisha utalii katika lile eneo.

Name

Allan Joseph Kiula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH aliuliza:- Kilwa ni moja ya miji mikongwe katika Afrika Mashariki tangu Anno Domino (AD) 900 -1700 pamoja na miji mingine ya Lamu, Mombasa, Sofala na Zanzibar. Miji hiyo ilipewa heshima ya jina la Urithi wa Dunia (World Heritage Site). Kwa kawaida miji hiyo husaidiwa na Mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani, Japan, Ujerumani, Uingereza na Shirika la UNESCO:- Je, Serikali ya Tanzania imefaidika nini kutoka katika Mataifa hayo yanayosaidia nchi za urithi wa dunia?

Supplementary Question 2

MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwa sababu yapo maeneo mengine ambayo yanaweza na yenyewe kuwa ni urithi wa dunia, kama vile magofu ya Mjerumani ya Mkalama. Wizara inafanya juhudi gani kuyaweka katika orodha hiyo na kuona namna ya kuyaboresha? (Makofi)

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Allan Kiula, Mbunge wa Mkalama, rafiki na kaka yangu ambaye tunalingana urefu, hongera sana. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kweli kabisa katika maeneo yale kuna magofu yaliyoachwa na Mjerumani. Katika utaratibu ambao Wizara sasa imeamua kuchukua, tumeamua kuangalia mali kale zote zilizopo na kuziboresha. Ili tuweze kuziboresha, hatua ambazo tumechukua, tumeamua kushirikisha hizi taasisi zilizo chini ya Wizara zenye uwezo kidogo wa kifedha na kuwakabidhi hayo maeneo ili waweze kutengeneza miundombinu mizuri iweze kusaidia katika kuboresha na kuyatangaza na kuvutia watalii katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika jitihada hizi, nina imani kabisa yale maeneo ya magofu yatapata ufadhili mzuri sana na hivyo yataimarika vizuri sana na kuweza kuvutia watalii.