Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Prosper Joseph Mbena

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. PROSPER J. MBENA aliuliza:- Nchi nyingi duniani ikiwemo Japan, Uholanzi na Marekani hutumia wataalam wastaafu kwenye sekta mbalimbali za uchumi katika shughuli mbalimbali za kutoa ushauri ndani na nje ya nchi zao. Wataalam hao (volunteers) wanatoa mchango mkubwa kwenye kushauri. (a) Je, ni lini nchi yetu itaiga utaratibu huo mzuri wa kuwatumia wataalam wake wastaafu ipasavyo badala ya kuwaacha tu mitaani? (b) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuweka kumbukumbu ya taarifa ya wataalam wastaafu wake (directory) kwa kila mmoja kwenye fani yake (profession) ili kuweza kuwatumia wataalam wastaafu hao pale ushauri wao utakapohitajika?

Supplementary Question 1

MHE. PROSPER J. MBENA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naomba niulize swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, Shirika la Chakula Duniani (FAO) ni moja kati ya wafadhili wa miradi hii ya kilimo kwenye nchi yetu na wanao mkataba maalum kwa wataalam wao wanaostaafu kuendelea kufanya kazi kati ya umri wa miaka 60 mpaka 70 na labda ni-declare interest tu kwamba mimi ni mstaafu, lakini nauliza swali hili kwa maslahi mapana ya nchi.
Je, kwa nini Serikali mpaka sasa haijasaini mkataba wa utumiaji wa wataalam (national experts) na Shirika la FAO wakati kuna nchi zaidi ya 67 wanachama wa FAO wameshasaini?

Name

Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MADINI (K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI UMMA NA UTAWALA BORA):
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa kwa niaba ya Serikali nimpongeze kwa namna ambavyo amekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha utumishi wetu wa umma, lakini zaidi kwa namna ambavyo amekuwa akifuatilia maslahi na mustakabali wa wastaafu wetu. Nipende tu kumwambia Mheshimiwa Mbunge kwa takwimu za mwaka 1995 mwezi Machi, ndipo ambapo Tanzania ilikuwa bado haijaweza kusaini mkataba huu.
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwaka 1998 Tanzania ilikuwa imeshasaini na kwa sasa hivi tunayo Technical Cooperation among Developing Countries pamoja na Countries in Transition na ninaamini Serikali itaweza kunufaika, lakini pia na wataalam wetu katika sekta mbalimbali, lakini nimshukuru kwa kuleta hoja hii na tutaendelea pia, kufuatilia na mikataba mingine ya kimataifa ili watu wetu waweze kunufaika.