Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yussuf Haji Khamis

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Nungwi

Primary Question

MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS aliuliza:- Kituo cha Polisi cha Mkokotoni kiliungua mnamo tarehe 27/12/2010 na ujenzi wake ulianza mara moja. Je, ni lini ujenzi huu utakamilika na kituo hicho kuendelea na shughuli zake?

Supplementary Question 1

MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri tuliyoyazoea, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, takriban tangu kuungua kwa kitu hiki ni miaka tisa na kipindi hicho chote askari wanafanya kazi katika mazingira magumu sana kiasi wanahatarisha afya zao. Kwa kuwa Serikali imeshindwa kukamilisha kituo hiki katia muda mwafaka, je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kukifunga kituo hiki mpaka ujenzi wake ukamilike kwa usalama wa skari wetu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetenga shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya kupunguza madeni ya wakandarasi. Kituo cha Mkokotoni kimetengewa shilingi milioni 200 kwa ajili ya mkandarasi aliyejenga kituo kile, nataka kujua, je, mkandarasi huyo ameshalipwa pesa zake? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi hatuna mpango wa kukifunga hiki kituo kwa sababu mipangilio ya kukiendeleza, kukikamilisha iko mbioni na ndiyo maana naomba nichukue fursa hii kumjulisha Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshafanya uhakiki na kuwasilisha Hazina ili mkandarasi aweze kulipwa na ujenzi uweze kukamilika. Kitakapo kamilika kituo hiki kitatumika. (Makofi)