Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Haroon Mulla Pirmohamed

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbarali

Primary Question

MHE. HAROON M. PIRMOHAMED aliuliza:- Katika GN. Na. 28 ya mwaka 2008 inawataka wananchi wanaoishi katika vijiji 21 vilivyopo katika Jimbo la Mbarali, Wilaya ya Mbarali, Mkoani Mbeya wahame ili kupisha Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ingawa wananchi katika vijiji hivyo wameishi katika maeneo hayo tangu enzi za mababu zao:- Je, ni lini Serikali itafuta GN. Na. 28 ya mwaka 2008 ili wananchi katika vijiji hivyo waweze kuishi bila kubughudhiwa pamoja na kuendelea na shughuli zao za kilimo na ufugaji?

Supplementary Question 1

MHE. HAROON M. PIRMOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika, katika jibu lake la msingi Mheshimiwa Waziri amesema Serikali iliunda timu ya wataalam kupitia upya mipaka iliyotangazwa ili kutoa mapendekezo kuhusu mipaka hiyo ya GN. Na. 28. Mheshimiwa Naibu Waziri anaweza kuliambia Bunge lako Tukufu kwamba zoezi hili litamalizika lini?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa mgombea Urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana aliwaahidi wananchi wa Mbarali wanaoishi katika vijiji hivyo 21 kumaliza kero hiyo na kwa kuwa mgombea huyo sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Je, Mheshimiwa Waziri kuendelea kuchelea kutoa jibu hili haoni kama anapinga ahadi aliyotoa Rais, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli?

Name

Eng. Ramo Matala Makani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa ni lini au ni baada ya muda gani zoezi hilo ambalo linakamilishwa na Kamati iliyoundwa litakamilika? Nimepitia taarifa ya awali ya Kamati hiyo ambayo tumesema inakamilisha kazi iliyopewa, napenda kukufahamisha kwamba kazi hiyo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja itakuwa imekamilika ikiwa ni pamoja na kwenda kufanya ukaguzi wa maeneo yanayohusika.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, pengine jambo muhimu si kuzungumzia zaidi kwamba kuna ukiukwaji au kuna utaratibu ambao unaonekana kupingana na ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais, jambo la msingi hapa ni kwamba kazi hii ni muhimu na suala la kushughulikia changamoto za wananchi pia ni ahadi ya Serikali hii ya Awamu ya Tano na katika kipindi hicho ambacho nimekisema suala hilo litakuwa limekamilika na kupatiwa uvumbuzi.