Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE M. LUBELEJE aliuliza:- Serikali ilikuwa na mpango wa kuchimba mabwawa katika vijiji vya Msagali, Bumila, Makutupa, Lupeta, Inzomvu, Vibelewele, Kimagai, Chunyu na Ng’ambi ambayo yatahudumia wananchi pamoja na mifugo na kilimo cha umwagiliaji. Je, Serikali imefikia hatua gani ya utekelezaji wa mpango huo?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri, niipongeze sana TASAF kwa kazi nzuri, sasa nina maswali mawili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza ni kwamba kazi hii kweli imeanza Mheshimiwa Naibu Waziri lakini bado haijakamilika katika vijiji ulivyotaja. Ni lini kazi hii itakamilika ili maeneo haya yaweze kupata huduma ya maji kwa sababu kuna shida kubwa sana ya maji?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali ina mpango gani wa kuongeza vijiji katika mpango wa kuchimbiwa mabwawa, katika vijiji vya Kisisi, Ngalamilo, Iwondo pamoja na Nana kwa sababu hawa nao wana matatizo makubwa sana ya maji. Ni lini wataanza shughuli hizi? (Makofi)

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lubeleje, Senior MP kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, lini miradi hii itakamilika na kuweza kutoa huduma ya maji, kwanza naomba nimuahidi katika Bunge hili la bajeti linaloendelea nitaomba mimi na Mheshimiwa Lubeleje twende katika miradi hii tukaiangalie kwanza halafu tushauriane vizuri tukiwa site kwa sababu najua Wilaya ya Mpwapwa ina tatizo kubwa sana la maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vijiji vingine ambavyo ameviorodhesha ni kweli, nafahamu maeneo kwa mfano hata kule Tambi hali ya maji ni mbaya mpaka wanakuja huku Chamkoroma kutafuta maji. Kwa hiyo, tuna kila sababu kuhakikisha kwamba Wilaya ya Mpwapwa tunaipa kipaumbele. Pia katika ziara yangu hii nikiwa na Mheshimiwa Mbunge tutaambatana na wataalam kutoka kwenye Halmashauri tuweze kufika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Makutupa ambako Mheshimiwa alikuwa anapigia kelele sana muda mrefu jinsi gani tutafanya kuweka mipango sahihi kusaidia shida ya maji katika Wilaya yetu ya Mpwapwa.